SOMO:Njia Za Awali Anazotumia Mungu Aliye Hai Kuwasiliana Nasi: - TopicsExpress



          

SOMO:Njia Za Awali Anazotumia Mungu Aliye Hai Kuwasiliana Nasi: katika eneo hili nitakueleza njia anazotumia Roho Mtakatifu kusema au kuwasiliana n na wanadamu. 1Korintho 2:13-15. Hakikisha unakaa katika hali ya maombi, unapoendelea, kusoma kitabu hiki. Ni maombi yangu na wewe, ufikie kuwa mwalimu mzuri zaidi kuliko hata mimi. Njia anazotumua Roho Mtakatifu kuzungumza na watu ni kama ifuatavyo:- i. Ndoto. ii. Njozi. iii. Maono. iv. Mafunuo. v. Dhamiri Safi. vi. Neno lenye ufunuo UFANUNUZI: NDOTO: Yeremia 23:22 Mara nyingi ndoto, hutokea wakati mtu amelala na amepumzika asilimia mia 100%, yaani usingizi mzito. Na mara nyingi hutokea wakati wa usiku wa manane saa sita mpaka saa tisa, au wakati wowote ule ambao utakukuta umelala usingizi mzito sana. Mwanzo 37:9… “Akaota ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake akasema, angalieni nimeota ndoto nyingine, natazama, jua na mwezi na nyota kumi na moja zikaniinamia” Yeremia 23:22…” lakini kama wangalisimama katika baraza yangu, ndipo wangaliwasikizisha watu wangu maneno yangu,na kuwageuza waziache njia zao mbaya, na uovu wa watendo yao” Yeremia 23:28… “Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na neno langu, na aseme neno langu kwa uaminifu. Jinsi ndoto inavyofanya kazi ulimwengu wa roho: Nabii anayefunuliwa kupitia ndoto anapata maneno haya Kama ifuatavyo; Mungu Aliye hai anapenda kutumia mfumo wa fikra ulio ndani ya mwanadamu, kupitisha ujumbe wa picha na sauti, kwa namna ya ndoto, ili kumtaarifu mwanadamu kuhusu tukio Fulani, litakalotokea maishani mwake au hapa duniani. Kwa hiyo unapo amka kutoka usingizini unatakiwa uombe Mungu ili kuzuia ile vita uliyoiona isitokee. NJOZI Habakuki 2:2 Daniel 2:28 Njozi hutokea wakati mwanadamu, ufahamu wake umepumzika nusu. Na mara nyingi hutokea kuanzia saa kumi asubuhi na kuendelea, au wakati wowote unapokuwa umelala usingizi mwepesi. Ndoto na Njozi zinafanana kidogo lakini ni katika maeneo mawili ukiota; kama unaangalia video ujue ya kuwa neno hilo litampata mtu mwingine na sio wewe. Lakini ukiota, na wewe ukiwa eneo la tukio; Lakini muda na masaa yaliyopendekezwa, yamewekwa baada ya kufanyika utafiti wa kina. Habakuki 2:2…”Bwana akanijibu akasema, iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao ili aisomae apate kuisoma kama maji. Mfano: Ukiota Unakimbizwa na mnyama mkali au unadondoka na kutumbukia shimoni, basi ujue wewe uliye ona yatakutokea, na kukupata. Kwa hiyo unapo amka kutoka usingizini unatakiwa uombe Mungu ili kuzuia ile vita uliyoiona isitokee. MAONO Maono ni jicho la rohoni, linaloona umbali wa wastani.Mfano: Miezi au miaka kadhaa ijayo au iliyopita. Ayubu 33:14, 15 Danieli 8:12-14…” Ndipo nikamsikia mtakatifu mmoja akinena,na mtakatifu mwingine akamuuliza huyo aliye nena, haya maono katika habari ya sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lini,kukanyagisha patakatifu na jeshi” muda na masaa yaliyopendekezwa, yamewekwa baada ya kufanyika utafiti wa kina. MAFUNUO: 1Korintho 2:6-10, Ufunuo 1:1, 10. Mafunuo ni jicho au macho ya rohoni, yanayo ona umbali mkubwa sana. Mtumishi yeyote anaweza kupewa macho ya aina hii na Roho Mtakatifu, kwa kusudi Fulani katika utumishi. Neno mafunuo ni lugha ya ki- biblia inayo maanisha macho ya rohoni, au uwezo wa kuona viumbe hai kutoka ulimengu wa roho, au mbinguni, au hata hapa duniani. Kila aliyemwamini Yesu Kristo anayo haki ya kupokea zawadi hii nzuri ya macho ya kiroho kutoka mbinguni. Ufunuo 1:1…”Ufunuo wa Yesu Kristo aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika, akamwonyesha mtumwa wake Yohana” DHAMIRI SAFI Matendo 23:1, 24:16,1kor 2:11 Dhamiri safi ni aina ya SAUTI ya ndani inayozungumza katika mtu wa ndani (audial voice and inner spirit). Sauti hii unaweza kuisikia eneo la kifuani karibu na chembe moyo (diaphragm) Matendo 23:1… “Paulo akawakazia macho watu wa baraza akasema, ndugu zangu, mimi kwa dhamiri safi kabisa nimeishi mbele za Mungu, hataleo hivi.” Matendo 24:16… “Nami najizoeza katika neno hili niwe na dhamiri isiyo na hatia mbele za Mungu na mbele ya watu siku zote”. Dhamiri safi inafanya kazi na ufahamu wa moyoni ndani ya mwanadamu. Ndani ya nafsi ya mwanadamu kuna hisia, akili na uwezo wa kuamua. Hii ni ndani ya mfumo wa kisaikolojia wa mwanadamu. Ndani ya dhamiri, kuna aina Fulani ya sauti ndogo inayozungumza (Inner voice inside Basic instinct of human being). Katika kifua cha mwanadamu ni eneo la chembe moyo. Kama ukiweza kutumika vizuri dhamiri safi, unakuwa fundi wa imani, yaani unakuwa na uwezo wa kuitawala imani yako vizuri, na kuitumia vema katika utumishi na maisha kwa ujumla. Ayub 33: 14, 23. Kuna aina Fulani ya malaika anaitwa; malaika mkalimani, huyu ndiye anayepeleka tafsiri, akili na ufahamu wa kupambanua , ule ujumbe wa sauti na ujumbe wa picha utakayoiona na kusikia kutoka ulimwengu wa roho. Ayubu33:23 “Kwamba akiwapo malaika pamoja naye Mkalimani, m’moja katika elfu,ili kumwonyesha binadamu hayo yampasayo NENO LA UZIMA Njia nyingine inayotumiwa na Roho Mtakatifu wakati mtumishi anahubiri madhabahuni. Roho Mtakatifu anampa mtiriko unaoendana na mahitaji ya watu hapo kanisani au kwenye maombi. Kwa mtumishi yeyote mwenye neema hii anaelewa ninasema nini, hasa kwa wale wanaosimama madhabahuni na kufundisha. UFUNUO WA NENO Hii ni ufunuo unaojitokeza wakati mwalimu anafundisha. Inaleta furaha ya Roho Mtakatifu Sana. Isaya 61:1-2… “Roho ya Bwana Mungu I juu yangu, kwa sababu amenitia mafuta, niwahubiri wanyenyekevu habari njema, amenituma kuwaganga waliovunjika moyo,kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari ya kufunguliwa kwao, kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao Ni aina ya ujumbe kutoka mbinguni, uliobeba majibu ya wale wanao sikiliza. Na baada ya hapo, inaleta maarifa ya hali ya juu, yanayoleta ufumbuzi na suluhisho kwa mahitaji ya watu, kwa njia ya Roho Mtakatifu wakati wa ibada. Udhihirisho Unaojitokeza Katika Huduma Ya Unabii: Mara nyingi unabii unapofanya kazi ujidhihirisha katika namna zifuatazo: 1. Kufunua mambo yaliyopita. Ufunuo3:3-5 “Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, Na jinsi ulivyo sikia, yashike hayo na kutubu” 2. Kufunua yaliyopo. Ufunuo 3:1,2 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko sardi andika haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba,nayajua matendo yako,yakuwa unajina la kuwa hai nawe umekufa” Hii ndiyo moja wapo ya jinsi unabii unavyotenda kazi. 3.Kufunua matukio yajayo na kuyaweka hadharani. Ufunuo 4:1 “Baada ya hayo, naliona, natazama mlango ukafunguka mbinguni, sauti ile ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu, ikinena name, ikisema, panda hata huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo” Mwanzo 49:1... “Yakobo akawaita wanawe akasema, kusanyikeni ili iwaambie yatakayowapata siku za mwisho”.
Posted on: Thu, 15 Aug 2013 16:43:04 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015