SOMO : Tahadhari Kwa Watumishi Wote: 1Thes5:19,20. Kwa - TopicsExpress



          

SOMO : Tahadhari Kwa Watumishi Wote: 1Thes5:19,20. Kwa wachungaji, Maaskofu na watumishi wote wa madhabahuni, nawatahadharisha kuwa, Ni marufuku kuuzimisha au kuutweza unabii. Badala yake unatakiwa uupime; kwa hekima na ufahamu, na mafunuo ya Roho Mtakatifu kama unayo neema hii. kama nilivyo elekeza hapo awali katika waraka wangu ndani ya kitabu hiki. Kwa kuwa siyo kila mtumishi anaweza kufundisha somo hili la kipawa cha Unabii. “Wengi wao” ni wakosoaji wazuri au wapingaji wazuri. Lakini ukiimuliza kuhusu somo hili, utakuta hana jibu sahihi, au hajui kabisa, zaidi sana atakupa jibu la kisiasa. Na kama amekuzidi umri na wewe ni kijani, basi hapa ndio taabu kwelikweli !. wengi wao wana misimamo ya zamani, hawataki kubadilika, wala hawataki maneno mapya kutoka mbinguni hasa kutoka kwa watumishi vijana katika makanisa mengi. Zingatia sana neno hili nikuambialo leo hii, Kama hauwezi, kuupima unabii, na hauna neema hii, nakushauri uliza wenzako wenye neema hii, wakusaidie. Ukifanya jeuri, na kutumia umri wako, au cheo chako kupinga au kuushambulia unabii, utakutana na ghadhabu ya Roho Mtakatifu. Kumb 11:1-5 Lakini wewe mtumishi, kama una nia ya kujua maneno haya nakushauri umwombe Roho Mtakatifu ili akusaidie kama utaweza. Maana yeye ndiye mwalimu mkuu aliye achiwa kanisa na Yesu ili alifundishe na kulifikisha kwenye kweli yote. Yohana 16:12, 13 “Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia,lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa. Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote;kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe,lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari zake Jukumu La Roho Mtakatifu Katika Malezi Ya Kipawa Cha Unabii: Jukumu la Roho Mtakatifu katika malezi ya kipawa cha Unabii, ni; kuhakikisha huduma hii haipingwi, na mwili wa Yesu Hapa duniani unapata maarifa ya kutosha. Lengo ni kuondoa ujinga katika maneno haya, ili kupata ufahamu. Maana kitabu cha Mwanzo kinaelezea vizuri mojawapo ya Kazi za Roho Mtakatifu kwa Kanisa la Yesu Kristo hapa Duniani kuhusiana na kipawa cha Unabii. Na maelezo yake ni kama ifuatavyo:- 1. Mwanzo 1:1-3…“Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa tena utupu na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji. Roho ya Mungu Ikatulia juu ya Uso wa maji.” Mungu aliye hai alimtuma Roho mtakatifu ili kuondoa yafuatayo:- i. Ukiwa ii. Utupu iii. Giza Haya ni mambo yanayowasumbua watumishi wengi sana hivi sasa. Na yanasababisha Kanisa kudumaa Kiroho na kurudi nyuma. i. UKIWA Ukiwa ni hali ya kukosa malezi ya kiroho katika utumishi. Maana msingi wa leo umejengwa jana na msingi wa kesho unajengwa leo. Watumishi wengi wa zamani au waliotangulia hawakuwa na walezi wa kiroho. Yaani hawakuandaliwa Ki-utumishi vizuri. Ndio maana na wao hawa hangaiki kuinua huduma chipukizi za Vijana Makanisani. Roho Mtakatifu ameamua kuchukua hatamu ya kusaidia wanaochipukia kihuduma makanisani hivi sasa. ii. UTUPU Utupu ni hali ya kufilisika kiroho na kukosa chakula cha kiroho cha uzima cha kushibisha roho za Watu. Mwalimu Mkuu wa maneno ya uzima ni Roho Mtakatifu Tafuta msaada wa Roho Mtakatifu ili upate chakula cha roho yako. iii. GIZA Giza ni ujinga wa kiroho unaotokana na kutokuyajua vizuri maneno ya kiroho au Neno la uzima lenye ufunuo wa Roho Mtakatifu Ayub 22:21-22…”Mjue sana Mungu ili uwe na Amani,ndivyo mema yatakavyokujia. Uyapokee tafadhali mafunzo yatokayo kinywani mwake. Na maneno yake uyaweke moyoni mwako. Hii ni kazi ya kwanza ya Roho Mtakatifu anayoifanya Mioyoni Mwetu. Isaya 63:10 Ina andikwa kuwa “Lakini wakaasi wakamhuzunisha Roho yake mtakatifu; kwa hiyo akawageukia akawa adui akakapigana nao”. Ukithubutu kumpinga Roho Mtakatifu anakugeukia na kukushambulia. Inapotokea hivi inamaana inazungumzia habari za kifo, kama mojawapo ya adhabu inayowapata wale wote wanaopiga vita huduma ya unabii. Swali ni hili unadhani hata mtumishi atakayekuombea wakati unaadhibiwa na Mungu ataomba kwa jina la nani ili upone?. Hili ni moja ya madhara yatakayo tokea kwa Mtumishi yeyote atakaye kiuka jambo hili. Na ni moja ya sababu kubwa sana inayofupisha maisha ya watumishi hapa duniani. sio ajabu, maana Elimu ya mambo ya kipawa cha Unabii kwa undani na ufunuo wa kina … RHEMA…, hayafundishwi katika vyuo vingi vya biblia. Kwa hiyo watumishi wengi hawamfahamu vizuri, jinsi kipawa cha unabii kinavyofanyakazi. Lakini hii haizuii kwa wao kupata adhabu kati pale wanapopinga fundisho hili la Unabii ambalo linasimamiwa na Ofisi ya Roho Mtakatifu hapa duniani.. NAMNA MCHUNGAJI ATAKAVYO WATUNZA WENYE HUDUMA YA UNABII Waumini wenye huduma ya Unabii wanatunzwa kama ifuatavyo:- i. Ni lazima uwe na hekima ya hali ya juu Daniel 1:17 ii. Unatakiwa uwe mtu wa rohoni mwenye nuru ya ufahamu. Efeso 1:17-18 1 iii. Uwe na mafundisho ya kuwafundisha wale wenye karama mbalimbali za Roho Mtakatifu 1Korintho 2:13.. “Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohono kwa maneno ya rohoni”. iv. Ni lazima uwe umejaa Roho mtakatifu vizuri Matendo 2:4-20 v. Ni lazima uwe na matunda ya Roho Mtakatifu Galatia 5:22,23 vi. Uwe na uzoefu wa kazi ya Roho vii. Uwe na nguvu na moto wa Roho Mtakatifu. Taratibu Za Kutoa Unabii Wakati Wa Ibada Au Maombi: Kwa wale wote wenye huduma hii ndani yao, naomba niwafundishe taratibu za kutoa unabii ili iwasaidie kwa faida ya mwili wa Yesu Kristo hapa Duniani. Sasa zingatia yafuatayo katka taratibu za kutoa unabii:- 1. Omba roho ya hekima, 1Timotheo 6:13-14. 2. Ukipata unabii wa mtu kutoka mbinguni, mjulishe mchungaji wako, kama una uhakika anayo, hekima. Mweleze ili yafanyiwe kazi. 2Timotheo 3:13—15 3. Acha tabia ya kufuatilia unabii ulioutoa na huku ukiimiza watu waufanyie kazi. Ukishakabidhi, waachie viongozi wako waufanyie kazi. 1Falme 18:1-2. 4. Ukipata neno la mtumishi yeyote, au anayekuzidi kiroho,usiseme hadharani, Bali nenda ukamwone faraghani. Maana ukimwaibisha, utapata hasara za kutisha kama adhabu kutoka kwa Roho Mtakatifu. Hesabu 12:1-10. 5. Jaribu kujidhibiti, unapojiliwa na nguvu za Roho Mtakatifu. Nyingi za Roho Mtakatifu, ili kuepuka kufanya mambo bila hekima. 6. Nenda kwa hekima na adabu unapoenda kupeleka unabii. 2Sam 12:1-8. 7. Tafuta hekima kutoka mbinguni ili umwelewe Mungu Aliye Hai vizuri, na ujue jinsi ya kwenda naye, na kuhojiana naye kwa hekima,ufahamu na akili ya mbinguni. Mathyo13;10-15 8. Epuka kuwadharau viongozi wa kanisa wanaokuchunga, maana itakuporomosha kiroho, badala yake onyesha utii na unyenyekevu. 9. Usiwadharau Manabii wenzako wachanga, wanaochipukia katika Huduma ya Unabii, badala yake, kaa nao karibu, wajenge, wafundishe, ili na wao wapige hatua hadi wafikie kukomaa kama wewe. 10. Kama inawezekana, andika kwenye daftari unabii ulioupata wakati wa maombi, kwa wakati muafaka utaufikisha kwa viongozi wa kanisa. 11. Kama umeona maneno magumu ya watu, kanisa au viongozi, uwe makini wakati unayasema, hasa mbele za waumini wachanga kiroho, ili usiwaangushe kiimani. 12. Epuka kutabiri maneno ambayo Mungu Hakukutuma, bali sema yale uliyotumwa tu, au uliyoyasikia kutoka ulimwengu wa roho. 13. Acha kutoa unabii wa kujipendekeza, ili upendwe na watumishi Fulani, bali, sema kweli ya Mungu Mtakatifu. 14. Unapotoa unabii, angalia usizidishe wala kupunguza kwa kutafuta sifa. 15. Kumbuka kurudisha utukufu na heshima kwa Yesu Aliyekupa kipawa cha Unabii . 16. Acha kujisifu kila mara, au ovyoovyo ili kujijengea jina isivyo halali kiroho, maana kipawa au karama, uliipewa kutoka mbinguni.
Posted on: Thu, 15 Aug 2013 16:47:01 +0000

Trending Topics



Officer
Vous êtes de plus en plus nombreux chaque jour a nous rejoindre
Eben an der Tankstelle......ein Herr steht neben mir und betankt

Recently Viewed Topics




© 2015