STORY FUPI ZA COX -- Kuna demu mmoja nilimuadd humu fb ukiangalia - TopicsExpress



          

STORY FUPI ZA COX -- Kuna demu mmoja nilimuadd humu fb ukiangalia picha zake lazima udate na alikuwa anajiita jina zuri sana la swaga linaendana na yeye alivyo kwenye picha zake Nilianza kujipendekeza kwake tukawa tunachat xana yani ikafikia hatua tukapeana hadi namba za simu tukawa tunapigiana sana sauti yake ilikuwa nzuri hadi nikazidi kupagawa kila mda nampigia simu ili niisikie tu nikamuuliza anapoishi akaniambia yeye anakaa Mbagala kwa dada yake Mwisho wa siku uvumilivu ukanishinda nikamtongoza bahati nzuri akanikubali nilifurahi sana kukubaliwa na kifaa kama kile nilitamba sana na kujisifia kwa masela japo sikuwahi kumuona live zaidi ya kumuona kene picha zake Siku moja nakumbuka ilikuwa jumapili yule demu akaniambia nimtimbie mbagala nikapajue kwao alafu na mimi nije naye home nilifurahi sana kusikia vile Nikategea broo katoka nikaiba jinsi yake kali na tisheti nikachukua na supra ya broo nikavaa juu nikatupia snapback nilipendeza sana nikajua lazima tu yule demu atanikubali na kuniona mkali Nilipanda daladala hadi mbagala nikafika nikampigia simu nimeshafika akaniambia nimuelekeze nilipo nikamuelekeza nikamuambia hadi nilivyovaa nimekaa pale nikaona kuna demu anaingia mweusiii amesuka mabutu nywele chafu ana matege demu ana misuli kama ananyanyua vyuma amevaa sketi ya tentemente na viatu aina ya bajaji Akaja nilipokaa akaniuliza "wewe ndo cox dawa yao?? Nikamwambia "ndiyo kwani wewe ni nani?? Akaniambia "jamani bby mm si ndo mpenzi wako tunaochat fb na kupigiana simu kila siku na ndo nimekuambia uje huku mbagala" nimechanganyikiwa kusikia vile nikamuambia "hapana sio ww mimi mpenzi wangu namjua hebu nitokee hapa mimi siwezi kuwa na mpenzi kama wewe" Yule demu akatoa simu akaanza kunuonyesha message tunazochatigi akaniambia "kweli bby ndo mimi zile picha fb sio zangu nimeweka za ndugu yangu anasoma kenya" nilijikuta jasho jembamba linanitoka nikasimama pale ile nataka kuondoka akanishika mkono akaniuliza "vipi bby mbna unaondoka?? Nikamwambia "shenzi mkubwa we hebu niachie mkono wangu mimi nimepoteza mda wangu kuja hadi huku kumbe mtu mwenyewe ndo wewe zile pic fb sio zako" Yule demu aalinirukia alinipiga ngumi ya uso alinikaba roba akaniambia"nyie makaka ya fb mnapenda sana kutongoza leo umeingia cha kike" demu alinikaba nilijitahidi kujitoa lkn nilishindwa nilianza kupiga kelele za kuomba msaada watu walijaa pale walijua mimi mwizi nilitaka kumuibia yule demu nilipata upenyo nilitoka nduki huku nipo kifua wazi uso umevimba tisheti ya broo snapback ya broo na supra vyote nimeviacha nilitembea kwa mguu hadi home huku nalia mm nilijua naenda kumchukua mrembo wangu wa ukweli kumbe majanga Nilifika home nikaingia fb nikamblock fasta yule demu anapiga ngumi kama dume broo alivyorudi akakuta vitu vyake havipo ndo ilikuwa balaa kichapo nilichopewa hadi leo nimekoma kutongoza mademu ovyo GONGA LIKE/SHARE/KAMA UMEIPENDA HII STORY
Posted on: Tue, 08 Oct 2013 08:34:50 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015