Sijawai ona msiri kama fb... hata uwe hujui kutumia computer - TopicsExpress



          

Sijawai ona msiri kama fb... hata uwe hujui kutumia computer anakuruhusu kumtumia kwa phone. anaruhusu mwanandoa kujiita yupo single, dada yupo kijijini sigimbi ila unamtambulisha eti yupo new york. dada anatembelea ndala(malapa) unamuwekea muonekano wa high hill, jamaa anasura mbaya kama kinyago unamuonesha bonge la handsome. wanaume wengine sikuizi unawaruhusu wakutumie kwa wadhifa wa kike. mtu kanuna ila unamuonesha kafurahia kitu flan. wengi hawajui hata kuwasha tv ila unawawekea status za kipindi flan cha tv. jamaa analala kitanda kimoja na kunguni, mende lakini unamuonesha kuwa anatumia kitanda kama cha 50 cent. dada wa kule nkunduchi village hajasoma hata cheke chea unamuonesha yupo university. dada mmoja anakiuno kama kitenvu unamuonesha kafanana na rihanna. watu wanatukanana inbox ila we husemi. umechangia jamaa kutoka nje ya ndoa kwa ukuhadi wako. unakubali jamaa kusema yupo kanisani au msikitini wakati yupo bar tena kalewa kama mlenda. kweli we facebook msiri sanaa
Posted on: Mon, 08 Jul 2013 17:48:34 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015