Sourc: Chadema in Blood ndugu watanzania, zimebaki siku kadhaa - TopicsExpress



          

Sourc: Chadema in Blood ndugu watanzania, zimebaki siku kadhaa kutimiza mwaka mmoja toka pale ndugu yetu daudi mwangosi alipouawa na polisi kwa bomu pale kijijini nyololo. Mwangosi aliuawa tar 02/09/2012 na hii ina maana tar 02/09/2013 ndio itakuwa ni siku ya kumkumbuka. Chadema wilaya ya mufindi tumeandaa shughuli mbalimbali kumkumbuka ndugu yetu. Jimbo la mufindi kusini wanaratibu shughuli hizo. Kutakuwa na matukio makubwa mawili 1. Uzinduzi wa mnara wa kumbukumbu ya mwangosi ambao utasimikwa na katibu mkuu wa chadema taifa ndg dr. Wilbrod slaa. 2. Harambee ya kuchangia familia ya mwangosi mchango ambao utawasilishwa kwa mjane wa marehemu siku hiyo 3. Mkutano wa hadhara utakao fanyika nyololo na igowole tunapenda kuwashirikisha wale wote ambao wangependa kuchangia shughuli zote hizo. Tunatoa namba za simu za makamanda wanaohusika na uratibu wa shughuli hizo a. Katibu jimbo, emmanuel ngwalanje 0787797950 b. Katibu mwenezi jimbo, elisha msemwa 0755733918 c. Mhazini jimbo, karolina kidenya 0768757447 karibuni wote
Posted on: Sun, 11 Aug 2013 15:47:30 +0000

Recently Viewed Topics




© 2015