TAMAA MBAYA. Superstar alipata pesa akaamua kuhamia mitaa ya watu - TopicsExpress



          

TAMAA MBAYA. Superstar alipata pesa akaamua kuhamia mitaa ya watu wenye pesa pamoja na mkewe na mtoto wao mmoja. Siku moja mtoto alipokua akicheza, akarusha jiwe likavunja kioo cha nyumba ya jirani. Wakaamua kumuomba msamaha jirani. Walipobisha mlango wakafunguliwa na jizee moja. Jizee: Karibuni. Superstar: Ahsante, Tulihamia huku hivi majuzi. Tumekuja kukuomba msamaha mtoto wetu amerusha jiwe likavunja kioo chako.Tuko tayari kukulipa fidia. Jizee: Hakuna neno. Mimi ni Zimwi. Nilikua nimefungiwa ndani ya chupa kwa zaidi ya miaka 100. Jiwe limevunja kioo na likavunja pia na chupa niliyokuwa nimo ndani yake. Sasa niko huru. Ahsanteni sana. Ombeni chochote mtakacho nitawapa. Superstar: Mimi naomba niwe billionaire. Jizee: Sawa kesho ukiamka utajiona billionaire. Mke: Mimi naomba mume wangu asipende mtu mwengine ila mimi tu peke yangu. Niwe mfanyibiashara maarufu. Jizee: Sawa, kesho ukiamka kila kitu kitakuwa sawa. Nawashkuru sana ila mimi nami niko na ombi moja. Superstar: Sema tu. Jizee: Naomba kulala na mkeo usiku wa leo tu, kesho hamtaniona tena, na hiyo itakuwa siri yenu. Superstar na mkewe wakajadiliana wakaona hakuna neno, itakuwa siri yao. Wakamkubalia ombi lake. Hawawezi kuacha utajiri uwaponyoke kiurahisi. Asubuhi ya siku ya pili baada ya Jizee kuenjoy usiku mzima na mke wa superstar, Mazungumzo yakaendelea. Jizee: Nimefurahi sana bibie. Mke: Karibu sana, hata mimi nimefurahi. Jizee: Una miaka mingapi? Mke: 28. Jizee: Na mumeo je? Mke: 35. Jizee: Nyinyi nyote ni watu wazima, hivi bado mnaamini stori za mazimwi!!!!!!!!
Posted on: Wed, 28 Aug 2013 10:23:40 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015