Tahariri ya BCMC kuhusu matusi ya Savula kwa Raila Hatua ya hapo - TopicsExpress



          

Tahariri ya BCMC kuhusu matusi ya Savula kwa Raila Hatua ya hapo jana ya mbunge wa Lugari Ayub Savula ya kumtusi aliekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga ni ya kusikitisha sana. Mara kwa mara vijana wamekuwa wakiomba wapewe nafasi ya kuongoza wakidai kuwa na ujuzi kuwaliko viongozi wazee, lakini tabia kama ya Savula inatia doa ari hiyo. Jambo ambalo tunataka Savula afahamu fika ni kuwa chochote anachotamka mahala popote kinachukuliwa kama usemi wa watu wa eneo lake la Lugari, kaunti ya Kakamega na mkoa wa magharibi kwa jumla. Ingawa huenda Savula alitaka kumfurahisha makamo wa rais William Ruto aliekuwepo, hatua hiyo ilimtokeza kama mbunge asie na uwezo wa kuakilisha wananchi na kuleta amani, umoja na maendeleo nchini. Wa aidha, tunataka mbunge huyu kijana, na aliekuwa mwanahabari wa jarida la Standard kufahamu kuwa sisi kama wanahabari tulipata aibu kubwa kutokana na matamshi yake na kuwa anafaa kuomba msamaha iwapo angali anazingatia maadini ya taaluma ya uandishi wa habari. Mwisho ni kuwa hata kama ana kisasi cha aina yoyote na Bw Raila, jambo la busara ni kuwa aende kwake binafsi na kutatua tofauti kati yao badala ya kumshambulia hadharani na kujiletea aibu ndogo ndogo kama zile alipata jana katika eneo la Aterait alipozomewa na wananchi na viongozi wa Busia hadi akaondoka kwenye mkutano kabla haujaisha. Ingawa alidai kuwa Bw Raila alianguka kura, jambo ambalo hafai kusahau ni kuwa zaidi ya wakenya milioni tano walimpigia kura, na hivyo basi alikuwa akiwakejeli wakenya hao akidhani kuwa anamtusi Raila. Na hiyo ndio tahariri yetu. * * * * *
Posted on: Sun, 30 Jun 2013 08:38:09 +0000

Trending Topics



409281">Monroe is still pretty unwell so we have just spoken to her

Recently Viewed Topics




© 2015