Tanga Sirudi Tena 14th January 2012, Jumamosi 12:00 noon Ama kwa - TopicsExpress



          

Tanga Sirudi Tena 14th January 2012, Jumamosi 12:00 noon Ama kwa hakika tukio lililomo kwenye simulizi hili ndilo lililonisababisha Mentor kuamua kutulia kama maji ya mtungi. Kwa kipindi cha kama miezi tisa hivi tangu Januari 2012 hadi Mwanzoni kabisa mwa mwezi Oktoba 2012 nilikuwa kikazi jijini Tanga kwenye kampuni moja ya BIMA ambapo tulikuwa tumefungua tawi jipya hivyo nikapelekwa kusaidia. Wanasema siku hizi sio, “Waja leo warudi leo” ni “Waja leo, kurudi majaliwa.” Tanga kuna kibao kimeandikwa, ‘Karibu Tanga’ unapoingia na tena, ‘Karibu Tanga’ unapotoka mkoani, watoto wa mjini wanasema, Utablow mapigo. Now… Katika kuhudumia wateja wangu siku hii nilikuwa ninaharakisha niweze kufunga ofisi mapema nikapumzike. Mara ghafla akaingia mdada mmoja shombe shombe hivi (nahisi huu ni ugonjwa wangu).Ghafla haraka zote zikasahaulika nikageuka kumhudumia tena kwa utaratibu wote. Aneth: Kaka habari ya saizi. Mentor: Nzuri tu mrembo, karibu. Aneth (Huku akitabasamu): asante, nahitaji kukata bima ya gari yangu. Mentor: Third party ama comprehensive? Aneth: Comprehensive. Yani iliisha tangu mwezi uliopita nimekuwa tu mzembe kukata mpaka nilipokamatwa na polisi asubuhi. Yani imenibidi nimtoe buku kumi kabisa. Si unajua leo Jumamosi gari likienda kituoni kutoka Jumatatu. Nikaona isiwe shida……….. [...akaendelea na maelezo yake marefu jinsi alivyokuwa na safari ya kumpeleka mtoto hospitali kisha arudi nyumbani kupika anaishi na mama yake na blah blah nyingi. Nami wala sikumkatisha kauli. Nikasahau appointment niliyokuwa nayo na Sue (Suzan...girlfriend wangu kwa wakati ule. Alikuwa amekuja Tanga kunisalimu kwa weekend ile) mchana ule. Basi Aneth akaendelea kuongea pale na hadi yasiyohusu BIMA huku nikimsikiliza kwa makini. Nikaja kugundua alikosa mtu wa kumsikiliza....] Nilimueleza vitu vinavyohitajika akaniahidi kuniletea Jumatatu ila akaniachia namba zake za simu ili niweze kuvifuatilia kwani ilikuwa kinyume na utendaji kuandika BIMA ilhali baadhi ya nyaraka za muhimu hazijaletwa. Jumatatu asubuhi nikamsindikiza Suzan stendi akapanda gari huyo akaenda zake Dar. Wakati narudi ofisini nikakumbuka ninatakiwa kumtafuta Aneth anipatie nyaraka zangu kwa ajili ya BIMA aliyokata. Nikampigia simu akaniambia yupo nyumbani bado na hana mpango wa kutoka ila alikuwa na kila kitu kama sina usafiri nichukue taxi atanilipa. Nikamwambia wala asijali anielekeze tu anapoishi nitafika. Kwa bahati nzuri nilikuwa nimehama na ka Duet kangu na kalinitosha kuendeleza uhuni wangu mtaani kwa watoto wa Kizugua. Huyoo mpaka Raskazoni ambapo wanaishi kwenye nyumba kubwa flani hivi. Nikampigia simu akaja kunifungulia geti huku kajifunga kanga tu. Natumai mtu mwenye imagination nzuri ataelewa mfadhaiko ulionipitia ghafla. Nikamsalimia ila akanitaka niingie ndani nami kwa shingo upande (ingawa kiroho niliingia kwa shingo nzima) nikazama ndani ya nyumba ya kifahari kiasi ambapo kwa ndani ilikuwa kama imegawanywa sehemu mbili kiasi kwamba familia mbili zinaweza kuishi bila kuingiliana kabisa. Aliniambia pale anaishi na mama yake. Nyumba yenyewe walikuwa wanaishi na mume wake ambaye kwa maelezo yake ya awali alifariki baada ya kupata ajali ya gari. Nikakaribishwa chai tukawa tunapiga stori za hapa na pale na kwamba ni miez sita sasa tangu afiwe na mumewe na kweli alikuwa anajisikia mpweke. Baadaye mwanaye aliamka akaja kunisalimia, anko Mentor. Very charming kid…Shaaban. Mida kama ya saa nne niliaga na kurudi zangu ofisini na kuendelea na kazi. Kuanzia siku ile tukawa tumeanza kuchat na kupigiana simu mara kwa mara. Upweke, wangu na wake, ulisaidia kuharakisha sisi kufahamiana haraka. Siku za weekend nilienda kumchukua yeye na mwanaye siku nyingine waje tu kwangu au twende forodhani kula urojo. Nyakati nyingine ilikuwa tu ni mimi na yeye tu hivyo mida ya jioni tulienda clubbing na starehe kama hizo. Mostly alipendelea kwenda La vida loca au Chichi club na alinidiscourage sana kwenda the famous La casa Chica jambo ambalo kwa kipindi kile sikujua ni kwa nini. Safari moja huanzisha nyingine. Tulikosa mambo ya kufanya pamoja na kama isemwavyo ‘Loneliness is directly proportional to the accumulation of proteins in the body.’ Na mimi protini zilianza kunielemea mwilini na Sue wangu yupo mbali nisingeweza kupata tulizo la moyo. Akili ya chini ikanituma kuwaza kwa nini nisijaribu kwa mrembo Aneth. Siku ya siku nikamkaribisha kwangu jioni nikamwambia kama vipi amwache kabisa mtoto kwa bibi yake maana baada ya hapo tungeenda club hivyo tungechelewa kurudi. Akakubali. Sikufanya masikhara nikajisemea moyoni liwalo na liwe. Nikaandaa DOMPO yangu vizuri na spaghetti kwa minced meat. Alinikuta nikiangalia movie ya “Salt” aliyo act mwanadada Angelina Jolie. Nakumbuka alinilazimisha ku-rewind movie ile tukaanza wote tena. Akasogea kwenye kochi nililokuwa nimekaa (kosa!) ili tuangalie vizuri lakini pia kwa kuwa ndilo lililokuwa position nzuri relative to the tv screen. A little cuddle…a touch here and there..and bang! It happened, on the couch. Haikuhitaji dompo wala nini. Kumbe na yeye alikuwa na hamu kama au zaidi yangu. Kosa kubwa tulilofanya ni kutokutumia kinga maana, well, kwangu sikutarajia ingekuwa rahisi vile na hata angekubali ingekuwa baadaye sana so ningekuwa nimeshajipanga jinsi ya kwenda kuzichukua chumbani. Nilipata wasiwasi zaidi kuhusu yeye kupata mimba kuliko wasiwasi wowote ule wa magonjwa. Infact, ana mtoto mwenye nguvu na afya. Yeye mwenyewe bado analipa kabisa..hawezi kamwe kuwa nao! Kosa baada ya kosa..na huo ukawa mchezo wetu. Na alikuwa mtamu balaa maana hata hamu ya Sue wangu ilipungua akiniambia nimtumie nauli namwambia asuburi tu ntarudi mimi. Kumbe nilikuwa nikipata penzi kwa shombe, Aneth. 2nd June 2012, Jumamosi Penzi letu lilizidi kunoga na kuvuka mipaka kwani licha ya yeye kuja kwangu kuna nyakati nilikuwa nikienda kwake (kwao) nacheza na aanko Shaaban weee akilala tu nahamia kwa mamaye. Na kwa kuwa siku ya kwanza tulicheza pekupeku ilikuwa kama mchezo na sikuuliza wala kukumbushia tena suala lile. Ikawa ni mwendo wa kuhesabu tarehe tu..niliogopa mimba kuliko ngoma! Mentor mimi… Ijumaa ya tarehe moja kama kawaida nilienda kumchukua kwake tukaenda zetu mjini kuzurura. Usiku tukaenda zetu club. Mida ya tisa hivi aliniambia anajisikia kuchoka hivyo turudi nyumbani na akataka twende kwake. Hivyo tukaelekea kwake nami nikalala huko. Asubuhi... Wakati natoka getini ghafla na mama yake akawa anatoka ndani kwake akaniona nikiondoka. Nikawahi kutoka ghafla nikarudishia geti haraka. Lakini kabla sijapiga hatua kuelekea mbali nikamsikia mama yake akifoka kwa sauti kali lakini yenye huzuni kwa mbali. Mama Aneth: Wewe mtoto ni shetani gani huyo kakuingia? Hata kama hujionei huruma basi waonee huruma watoto wa wenzio. Mh! Akili ilitaka kuwaza kama The Boss (smartly) lakini nikaikataza na kuamua kuwaza ki- Boflo. Lakini ni kama nilikuwa ndo nafunguka macho. Nilipitia duka ambalo nilikuwa nanunua condoms kwa zile siku nilizokuwa natumia na Aneth (kuepuka mimba..danger days!) nikamsalimia muuzaji ambaye hadi wakati huo alikuwa ameanza kunizoea. Akanitania, “Duh, ila we jamaa una moyo.” Ah! Nikashtuka tena..nikamuuliza kwa nini? Muuzaji: “Yani mimi nkishajua demu kaukwaa hata nivae condoms ngapi siwezi kumgonga” Hee…nilipata kizunguzungu cha ghafla ila nilijikaza kisabuni na kununua zangu dawa na kusepa bila kumsemesha chochote. Kichwani nilijiuliza maswali mengi sana weekend ile, “Ina maana Aneth Kaathirika?” “Mbona hakuwahi kuniambia?” “Lakini hata sijawahi kumuona akimeza dawa!” “Mbona mwanaye anaonesha kuwa na afya tu?!” “Mama yake alimaanisha nini?” “Au ni kweli?” “…” Majibu yake nilianza kuyapata polepole kwani jioni ile ile nilimpigia aje nyumbani akaniambia atafika. Nilijidunga dozi za kutosha za Govinder kumar. Nikiwa tayari na vipimo vya HIV ili akija tupime wote. Alipofika wala sikumchelewesha nikamwambia lengo la kumuita bila kuhoji maswali. Akanikatalia katu katu kuwa hatopima. Kichwa kilitaka kunipasuka. Nikawaza mipango yangu yote na ndoto zangu zote za maisha zikanipitia zote kichwani ndani ya sekunde moja. Nilijiona nisiye na bahati. Aneth akaondoka kwa hasira tena akibamiza mlango kitendo kilichonishtua kutoka kwenye dimbwi la mawazo nililokuwa nimeanza kuzama. Kujipima mwenyewe nilishindwa…nikabaki navitazama vipimo vile huku nikikosa cha kufanya. Wiki iliyofuata ilikuwa ya ufunuo juu ya huyu mrembo Aneth ni nani hasa. Kumbe watu walikuwa na faili lake na hawakuniambia. Sasa ndipo nilipoanza kujua. Kweli niliamini hata binti awe mpole vipi, mrembo vipi usimuamini kirahisi hivyo. Kuna mengi nyuma. Nilikuja kufahamu kuwa mume wa Aneth alifariki kwa ugonjwa huo huo ila kwa kuwa alikuwa na pesa hata kwenye mazishi yake ilisemekana ni ajali aliyopata akiwa safarini kuelekea kwao Uarabuni. Nikahaikishiwa kuwa Aneth naye ameathirika baada ya kupewa ushahidi wa kutosha na kwamba anatumia vidonge vya kurefusha maisha (ARV’s). Nilijiaminisha kuwa nimeathirika. Nikakumbuka kiwanja changu nilichonunua miezi miwili iliyopita na kuwaza nyumba niliyotaka kujenga mwisho wa siku nitahitaji tu ukubwa wa futi sita chini na upana hata mita moja ungetosha kwa jinsi nitakavyokuwa nimekonda. Nilimuhadithia rafiki yangu Ceasar kisa chote na kumwambia endapo nitafariki basi aliyeniua ni huyo, Aneth. Niliishi kwa hali hiyo ya mawazo hadi kupoteza kilo kadhaa lakini kamwe sikufikiri kwenda kupima. Nilijua tayari ninao. 8th August 2012, Jumatano Sikukuu ya nane nane. Niliamka zangu mapema kuelekea viwanja vya mkwakwani kwani ndipo maonesho ya nane nane kwa mkoa wa Tanga yalipokuwa yakifanyika. Nami kwa kuwa nilikuwa na kibanda huko ilinipasa kuwepo mapema kabisa hivyo nilifika pale na kuandaa mazingira na kukaa kusubiri wageni. Kibanda cha pembeni alikuwa amekaa mdada mmoja mrembo, aliyejitambulisha kwa jina moja la Hollo. Tukazoeana haraka tukawa tunapiga stori juu ya maisha na kazi kwa ujumla. Kibanda chake kilikuwa cha ushauri nasaha na kupima virusi vya UKIMWI. Akaanza kunipa somo pale huku moyoni nikijua kwa nini nakataa kupima. Mwisho wa siku instinct za kiume zikaniingia nkamwambia kama ni kupima basi tupime wote. Hollo akakubali. Ni mwaka sasa Mentor ninaishi kwa matumaini baada ya kugundulika kutokuwa na virusi vya UKIMWI. Ila tukio lile lilinifanya niache uhuni. Leo nimepokea simu ya Aneth akinitaarifu kuwa anaumwa sana akidhani na mimi nimeathirika kama yeye. Nimemtia moyo tu na kumtaka azingatie maagizo ya daktari. Wasalaam wapendwa, Mentor.
Posted on: Tue, 08 Oct 2013 08:00:10 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015