" U P E N D O " ................Mwalimu, katika torati ni amri - TopicsExpress



          

" U P E N D O " ................Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu ? Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Katika amri hizi mbili hutegema torati yote na manabii. Mathayo 22: 36-40. .................Sasa yanadumu haya matatu: "IMANI TUMAINI NA UPENDO"; LAKINI LILILO KUU KUPITA YOTE NI " UPENDO"--1 Cor. 13: 1-13. U P E N D O : Maana yake ni nini ? Upendo maana yake ni "KUISHI KWA KUZITII AMRI ZAKE MUNGU". 2 Yohana 1 : 6. Wakristo wa kweli na waaminifu, ni lazima tuishi kwa kuzingatia "UKWELI NA UPENDO"; Hayo mawili yamaanisha kuwa waumini wa kweli na waaminifu tunapaswa kuishi kwa "UTII" yaani kwa "KUSHIKA AMRI ZA MUNGU". kama ushuhuda wa imani, tumaini na upendo wetu tulio nao kwa Baba yetu wa mbinguni na kwa wanadamu wenzetu :Kut. 20: 1-17; 34: 27-29; 19: 5,6; Yohana 14: 15-23; 15:10,14. "MTU AKISEMA KWAMBA ANAMJUA, LAKINI HAZITII AMRI ZAKE, BASI MTU HUYO NI MWONGO, NA UKWELI HAUMO NDANI YAKE"..1 Yohana 2: 3, 4; Yakobo 2: 10,11; Tito 1:16; Mathayo 5:19. NA AMRI YAKE NDIYO HII: TUMWAMINI MWANAE YESU KRISTO........NA KUZITII AMRI ZAKE. 1 YOHANA 3: 22-24; 5:2-4; Ufu. 14:12; Mhu. 12:8-14. TUKIZITII AMRI ZA MUNGU BABA YETU TUNAISHI KATIKA MUUNGANO NA MUNGU BABA YETU NA MUNGU BABA YETU ANAISHI KATIKA MUUNGANO NASI....Yohana 14: 21,23. Biblia yatufundisha ya kwamba tusiwe na deni kwa mtu ye yote, isipokuwa tu "DENI LA KUPENDANA". AMPENDAYE JIRANI YAKE AMEITEKELEZA SHERIA". Maana, " AMRI HIZI": Usiuwe; Usizini; Usitamani; na nyingine zote, zimo katika amri hii moja: " Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe. Ampendaye jirani yake hamtendei vibaya. Basi, upendo ni utimilifu wa sheria...Warumi 13: 8-10; 5: 1-10. Hapo Bwana alipokuwa amekwisha zungumza na Musa katika Mlima Sinai, "AKAMPA HIZO MBAO MBILI ZA USHUHUDA, MBAO MBILI ZA MAWE, ZILIZOANDIKWA KWA CHANDA CHA MUNGU BABA". Kutoka 31: 18; 34: 27-29; Yakobo 2:10-26. KWA HIYO NI LAZIMA KUTII, SI TU KWA SABABU YA KUOGOPA GHADHABU YA MUNGU BABA, BALI PIA KWA SABABU DHAMIRI INADAI HIVYO........2 Wakorintho 5: 14,15; Yohana 13: 34,35; 15: 9-17; 1 Sam. 22, 23; Mwanzo 22: 15-18. BABA YETU WA MBINGUNI: Ambaye zamani zilizopita alituacha mataifa yote, tuenende katika njia zetu wenyewe...LAKINI HAKUJIACHA PASIPO USHUHUDA.........Matendo 14: 16,17. Hivyo basi, nasi pia ni lazima tuwe na ushuhuda wa I M A N I , T U M A I N I NA U P E N D O wetu kwa Baba yetu wa mbinguni na kwa wanadamu pia. KWA SABABU MUNGU BABA WA MBINGUNI NI " U P E N D O " 1 Yohana 4: 7-21; Matendo 14:15-17.
Posted on: Thu, 01 Aug 2013 10:46:09 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015