UREMBO NA MAISHA KWA DADA ZETU. Nitoe tu mtazamo wangu na huu - TopicsExpress



          

UREMBO NA MAISHA KWA DADA ZETU. Nitoe tu mtazamo wangu na huu ujana na urembo na hizo rangi mnazo paka machoni dada zetu ambazo wengi wenu mwaona ni fashion kumbe kwa mtu mwenye akili timamu na mwenye kujitambua huwezi kuta amepaka hayo marangi. 1. Unajua wanatumia chemical gani kuzitengeneza.( hadi ifiikie we kuzipaka machoni tena karibia na mboni au kope) 2. unapaka leo baada ya miaka kumi uanze lalamika hauoni na uanze sumbuka maospitalini kutafuta tiba. 3. Jijengee tabia ya kuukubali urembo wako mungu aliokujalia na jione kuwa we ni mzuri haina haja ya kujikandika marangi hayo kwenye kope Angalizo : sio kila fashion lazima uende nayo mengine unayaacha yaende na unajaribu tunza na kuujali uzuri,utu na muonekano wako. Itafika siku utaambiwa utoboe jicho na we utafwata maana usione kitu wataka fanya!! Sorry kama nitamkwaza yeyote. Ila twasema haya maana tunawajali na kuwapenda.
Posted on: Tue, 30 Jul 2013 18:34:40 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015