Vituko vya J vyahamia H Na Ignatious Isigi Mmmh!Ukiona cha - TopicsExpress



          

Vituko vya J vyahamia H Na Ignatious Isigi Mmmh!Ukiona cha mwenzako kikinyolewa chako tia maji.Ni dhahiri shahiri kwamba shida za jumba la J zimeanza kuguria H.Huenda maghulamu wa H wanatafuta wapenzi huko J .Pengine mikosi ya J inapojaribu kurekebishwa huulizia pa kuenda.Bila shaka nikiulizwa swali hili nitalijibu ni katika jumba la H. Mbona nguvu za umeme zinapotea katika H pekee?Kulingana na utafiti niliufanya kwa siku tatu ,ni wazi kuwa taa zote huzima ifikapo saa mbili usiku na kurejea mnamo saa tatu unusu.Huenda kuna kitendawili ambacho chafaa kiteguliwe kulingana na haya.Labda kuna kile kitendekacho kwa takriban saa moja unusu katika jumba hili ambalo bado hakijajulikana. Wanaoteseka ni wale wanaopenda kupika mwendo wa saa mbili maadam inawabidi wangoje hadi umeme urudi.Bila shaka kwa wale wasiostahimili hubidi watafute njia mbadala ya kushtaki njaa.Swali ni je,mbona taa zinawaka vizuri mchana ilhali zizime usiku tu?Hili ni swali la kawaida lakini linanitia atiati. Kilio cha wale wenyeji wa H ni kurekebishwa kwa hali hii.Labda ni tuzo kwa maghulamu kwa kuwacheka mabanati wa J. Jambo jingine la kushangaza huko H ni kelele za usiku.Mchana kumetulia ilhali usiku utadhani ni danguro.Ni kama wengi wa maghulamu hukumbuka wana redio na runinga usiku tu.Siwalaumu pengine waliposoma ‘‘The Green Book” walielewa hivo .Basi kwa moyo mkunjufu nakuomba unayesoma maandishi haya kuongea nao labda kwa lugha ya mama-pengine wataelewa
Posted on: Fri, 29 Nov 2013 09:06:06 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015