Wabunge wetu naona leo wamuamua kutuvua nguo waandishi wa - TopicsExpress



          

Wabunge wetu naona leo wamuamua kutuvua nguo waandishi wa habari,wanajadili mabadiliko ya sheria mbalimbali,moja ya sheria hizo inatuhusu waandishi wa habari,inapendekezwa kuongeza makali ya adhabu dhidi yetu,wanapendekeza mbali ya sharia kali zinazotukandamiza,wanataka mwandishi wa habari ukikosea ufungwe miaka mitatu na adhabu ya shilingi Milioni Tano!nimemuangalia Pindi Chana,yeye ni mwanasheria analalamika na kuonyesha chuki na kukerw!...Pindi analalamika kuwa waandishi wamekuwa a nasi wanahabari,anadai waandishi wanawachafua watu!Yaani wabunge wetu wameamua kuongeza makali ya sheria dhidi ya waandishi wa habari!tunalalamikia uwepo wa sharia ya usalama wa taifa(1970),sharia ya magazeti(1976),sharia ya magereza(1967),sheria ya uchaguzi(1995),sharia namba 11 ya rushwa(2007),najiuliza sana kwa nini serikali inaamua kutunga sheria zenye hasira dhidi ya wanahabari?sijui kama wanayajua mazingira ya taaluma hii,ninavyofuatilia mjadala huu,wengi hawana uelewa na taaluma ta habari,wamejaa ubabe,wanasahu wao wanavyotumia ibara ya 100 ya katiba,inayowapa kinga kushambulia watu wasio ndani ya bunge,kwa kutumia ibara ya 100,baadhi ya wabunge wamekuwa wanawatuhumu watu walio nje ya bunge,je Pindi Chana,na wenzake,wameona tatizo la kuwashambulia watu lipo kwa wanahabari?wabunge nao wajiondolee kinga ya inayowapa jeuri ya kuwaumiza watu wakiwa maeneo ya Bunge!kwa nini serikali na Bunge waamue kuwaumiza waandishi wa habari bila kujua mazingira ya wanahabari?
Posted on: Wed, 06 Nov 2013 14:35:48 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015