Wanaume wawili nchini Kenya wameibuka na mbinu isiyo ya kawaida - TopicsExpress



          

Wanaume wawili nchini Kenya wameibuka na mbinu isiyo ya kawaida ya kupata suluhu ya kupigania mwanamke ambaye wote wanampenda Wamesaini mkataba wakikubaliana kuishi nae kwa zamu. Silvester Mwendwa ni mmoja wa wanaume hao anayeanza kwa kueleza kwa nini binafsi anamuhusudu mwanamke huyo. Mmoja ya wa wanaume hao alisema haoni ubaya wowote kwa yeye na mwenzake kumuoa mwanamke mmoja. Amehoji sheria ya sasa inayoruhusu wanaume kuoa wanawake wengi na wakati huo huo kuharamisha mpango kama huo kwa kina mama. Sylvester Mwendwa anasema wazazi wake wamekubali na mpango wake na wakotayari kumtolea mahari. Wanaume hao wawili walikubali kumuoa mwanamke huyo baada ya kugundua kwamba kumbe wote wana uhusiano wa kimapenzi naye. Na kumbe mwanamke huyo alikuwa ameahidiana na kila mmoja wao kwamba angelifunga nao ndoa bila ya wao kujuana. Lakini walipogunduana , ilikuwa ni ugomvi wa mara kwa mara lakini mwanamke huyo alipoambiwa amchaguwe mnmoja wao alishindwa akisema anawapenda wote wawili. Na baada ya hapo watatu hao waliafikiana kusaini mkataba ambao utaruhusu wanaume hao wawili kuishi na mwanamke huyo kama bwana na bibi ila kila mmoja wao atakuwa na wakati wake wa kwenda kumjulia hali. Vile vile mkataba huo unawashurutisha kugawana majukumu yote ya nyumbani ikiwa ni pamoja na kuwalea watoto na kutowabagua kwa kuwa wote watakuwa na haki sawa. Hata hivyo kwa mujibu wa sheria za kenya ni haramu kwa mwanamke kuolewa na wanaume wawili na mkataba huo sasa umeibua mjadala mkali wa kisheria, huku sheria mpya ya ndoa ikitarajiwa kujadiliwa na kuidhinishwa bungeni.
Posted on: Mon, 26 Aug 2013 14:38:55 +0000

Trending Topics



le="min-height:30px;">
En liten innrømmelse først: Jeg grugleder meg til kl. 21:00 i
Assurance IT - Oportunidades ABAP Sênior - Rio de
Entire Pakistan know Imran Khan and Dr. Tahir ul Qadri have the
Please could you post this anonymously: Hello. Im looking for a
Showstoppers Meeting Wednesday Jan 7th, 7:00PM I was going to
6th Place (Pink) Award Ribbons w/Card & String Latest reviews
Gerber 31-001794 Bear Grylls Intense Torch CLICK TO GET LOWEST

Recently Viewed Topics




© 2015