"YANI MI NI ZAIDI YA MSHUMAA" Namba - TopicsExpress



          

"YANI MI NI ZAIDI YA MSHUMAA" Namba xxxiv Niliongeza mwendo wa gari yangu ili tu niwahi kufika nilipokuwa naelekea sababu tulikuwa na nyumba nyingi za kuthaminisha siku ile "Hodiiii..........."Rafael alipisha hodi tulipofika kwenye ile nyumba iliyokuwepo maeneo ya Tabata karibu kabisa na hoteli kubwa iliyokuwa ikiitwa GREEN NIGHT,,dakika chache baadaye geti la nyumba ile likafunguliwa "Karibuni sana........."Kijana mmoja aliyekuwa na umri wa miaka kama ishirini na mbili na kuendelea alitukaribisha "Asante sana........."Niliitikia huku mi nikiwa wa kwanza kabisa kuingia ndani ya nyumba ile "Mama yako tumemkuta........?"Nilimuuliza kijana yule aliyekuwa amevaa bukta fupi na juu hakuwa na shati wala nini "Mama ametoka,,karibu sana....."Kijana yule alinijibu huku akionekana kuwa na wasiwasi zaidi na sisi "Tunaomba bili ya umeme mliyoilipia mwezi huu"Nilimwambia kijana yule,,mala moja kijana yule akaingia ndani na baadaye alitoka akiwa na bili niliyoihitaji mkononi!! Niliiangalia vizuri bili ile kufananisha majina na ile hati ya nyumba nikaona yanaendana kabisa "Embu angalia vizuri anataka mkopo wa bei gani........?"Nilimuuliza dada mmoja aliyekuwa amebeba mafaili yangu "Milioni tano.........."Dada yule alinijibu "Anapata kabisa..........."Niliongea huku nikigeuka nyuma kutaka kuanza kuelekea lilipo geti kwa ajili ya kutoka nje nilipoiacha gari yangu "Aaaaaaah Anitha.........."Nilishtuka kumuona Anitha akiingia ndani ya nyumba ile Anitha mwenyewe alionekana kunishangaa sana yani kama mtu ambaye hajategemea kabisa kuniona eneo lile,,wakati natembea kuelekea alipokuwa amesimama Anitha nilimuona yule dogo akinipita kwa nguvu na kwenda kumkumbatia Anitha tena kwa mabusu moto moto "Mungu wangu............"Sikuamini nilichokuwa nakiona,,mikono yangu ilikuwa kichwani huku nikiwaangalia walivyokuwa wanakumbatiana "James embu niachie tafadhali....."Anitha alimwambia yule kijana kisha akajitoa kwenye mwili wake na kunifuata nilipo "Wilbat mpenzi wangu naomba unisamehe........."Anita alinipgia magoti huku akitokwa na machozi "Naomba tusahau yote yaliyopita na tuanze upya"Anitha aliendelea kuniomba msamaha huku yule dogo aliyekuwa akiitwa James akishangaa Wafanya kazi wenzangu wote walikuwa kimya wakiniangalia,,mwili wangu ulikuwa ukitokwa na jasho jingi kiasi cha kunilowanisha nguo zangu zote nilizokuwa nimezivaa mala geti likafunguliwa tena akaingia mama aliyeonekana kuwa mwenye nyumba ile "Enheee kuna nin tena jamani.......?"Mama yule aliuliza kwa mshangao baada ya kumuona Anitha amepiga magoti mbele yangu "We James kuna nin kinachoendelea hapa?"Mama yule alimuuliza mwanaye kwa sauti ya ukali Kabla James hajajibu chochote mam yule alimuona Rafael,,akamsogelea "Vip baba kuna nini kwani.......?"Mama yule alimuuliza Rafael "Sijui huyo binti na bosi wetu......"Rafael alimjibu mama yule Moja kwa moja nikahisi kitu,,James alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Anitha na walikuwa na ahadi ya kuonana siku ile kwakuwa mama yule hakuwepo nyumbani "Rafael kama huyo ndo anayehitaji mkopo mwambie hawezi kupata aende kutafuta kwenye makampuni mengine"Niliongea kisha nikaondoka nikamuacha Anitha amepiga magoti chini!! *********** "Una nini Wilbat wangu...........?"Magreth aliniuliza alipoingia ofisini kwangu "Aaaah sipo pouwa tu nahisi naumwa"Nilimdanganya Magreth "Pole sana mpenzi,,twende nikupeleke hospital basi......"Magreth aliniambia kwa sauti ya upendo "Usijali,,nitakuwa sawa mana tayari nimeshakunywa panadol kwa ajil ya kupinguza maumivu"Nilimwambia Magreth "Wakina Rafael wako wapi.......?"Magreth aliniuliza baada ya kugundua nilirudi peke yangu bila ya watu niliokuwa nimeenda nao "Wapo njiani wanakuja........."Nilimjibu Magreth kisha nikainamia chini ya meza yangu nikaanza kumfikilia Anitha "Bila shaka atakuwa ana pepo la ngono......."Niliwaza huku nikikumbuka siku ya kwanza nilipomuona mwanamke yule "Lakini inawezekana anafanya hivyo sababu ya maisha tu"Niliendelea kuwaza huku nikihisi kitu ndani ya moyo wangu "Kwakweli siwezi kulifumbia macho jambo hili,,nahisi kabisa naweza kumsaidia Anitha akaacha kabisa tabia yake ya umalaya"Niliwaza huku nikiikumbuka sura ya upole ya Anitha "Kama nikijitahidi kuwa karibu na Anitha naamini ataacha kabisa mambo haya anayoyafanya sasa"Niliwaza huku nikichukua simu yangu nikiwa na lengo la kumpigia Anitha "Naomba nipishe ofisini tafadhali"Nilimwambia Magreth kwa sauti ya ukali ni wazi nilikuwa kama nimechanganyikiwa Mala ghafla mlango ukafunguliwa na Anitha akaigia ndani ya ofisi yangu,,uso kwa uso na Magreth kidume nikabaki nimeduwaa!! *********** Itaendelea Kesho................. Nawashukuru wote mnaoniunga mkono kwa kunitumia pesa na kusoma stori zangu zilizokuwa kwenye Magroup yangu Jiandaeni kusoma "JAMANI NYIE BABU KISUNUNU" Naombeni Maoni na Ushauri Wenu Juu Ya Simulizi Hii Ya Zaidi Ya Mshumaa Like Na Comment Za Kutosha Zinahitajika Na Kwa Maelezo Zaidi Waweza Kuja Inbox By #Hajrat
Posted on: Thu, 03 Oct 2013 08:29:10 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015