"YANI MI NI ZAIDI YA MSHUMAA" Namba - TopicsExpress



          

"YANI MI NI ZAIDI YA MSHUMAA" Namba xxxxi "Nimetoka kugombana naye mda si mrefu"Nilimjibu mama huku nikilia "Mbaya zaidi nimempiga mbele za watu,,sijui kama atanisamehe kwa kweli"Niliongea huku nikiendelea kutokwa na machozi,,makamasi yakaanza kunitoka kwa wingi,,ghafla nilimuona mama akitoa tenge alilokuwa amejifunika na kuanza kunifuta machozi na makamasi "Inuka mwanangu nimeshakusamehe........"Mama aliniambia kwa upendo,,ama kweli uchungu wa Mwana Haujuaye Ni Mama Pekee "Basi baba usilie nyamaza enheeee........"Mama alikuwa akinibembeleza kama mtoto mdogo "Wewe ni mwanaume mwanangu lazima uwe na moyo wa chuma"Mama aliniambia kwa sauti ya chini "Jifunze kuwa na #Mapenzi_Ya_Dhati kwa anayekupenda na si kila mwanamke mzuri basi atakupenda kama unavyodhani"Mama aliniambia maneno yaliyoanza kuniingia akilini "Anitha hakufai mwanangu............"Mama aliniambia huku akiniangalia usoni "Mwanamke mzuri ni yule ambaye ukiwa naye mambo yako yanakuwa mazuri,,lakini ukiona unampata mwanamke kisha mambo yako yanaenda vibaya ujue huyo hakufai"Mama aliongea kwa sauti kidogo "Wewe na Anitha nyota zenu haziendani kabisa ila we unafosi na ndomana mikosi haikuishi"Mama aliyeonekana kuwa na uchungu sana na mimi aliendelea kuongea "Fanya kitu kimoja kabla hujaingia chumbani kwako........"Mama aliniambia huku akiniangali usoni "Nenda kaoge maji ya bahari ili mikosi yote iishie huko uanze upya kabisa"Mama aliniambia huku akiingia chumbani kwangu Dakika tatu baadaye mama alirudi akiwa na suruali yangu pamoja na shati,,akaviweka kwenye mfuko kisha akanikabidhi "Ukishaoga utavaa nguo hizi,,hizo utaziacha ziondoke na maji"Mama alinipa maelekezo kisha akaelekea chumbani kwake kwa ajili ya kunitolea nauli!! *********** Nilifika salama Coco Beach,,nikaenda sehemu ambayo haikuwa na watu wengi nikavua nguo na kuanza kuogelea,,baada ya kuoga kwa muda mrefu nikatoka ndani ya maji na kuvaa nguo alizonipa mama "Wacha nimsikilize mama yangu tu ili nione itakuwaje........"Niliwaza wakati nikianza kutembea kuelekea nje ya Beach ile maarufu sana Jijini Dar es salaam!! Nilitembea pembezoni mwa maji nikiwaangalia warembo wazuri wazuri wakiogelea na wapenzi wao,,wapo ambao walikuwa wakiogelea peke yako,,wengine niliwaona wakiwa wamekaa kwenye michanga wakipiga stori hakika nilivutiwa sana na mazingira yale "Enheee mpaka #Masugar_Mamy wapo........!"Nilishangaa nilipoona wamama watu wazima wakiwa wanapunga upepo kando ya bahari,,kwakweli nilianza kusahau mateso niliyoyapata sero ndani ya masaa machache sana kwa kuwaangalia watu waliokuwa wanapenda kujiachia ifikapo mida ya jioni!! Taratibu nikaendelea kutembea hadi langoni kabisa mwa lango la kutoka nje ya Beach ile "Aaaaaagh........"Nilishtuka nilipomuona Anitha akiingia ndani ya Beach ile akiwa na mwanaume tena mbaya zaidi walikuwa wameshikana viuno "Anitha mpenzi wangu mbona unanichanganya............?"Nilijikuta nikiongea kwa sauti hafifu,,sauti iliyoashiria nipo kwenye maumivu makali sana ya mapenzi "Nifanye nini ili uamini kama nakupenda na nahitaji uwe wangu peke yangu?"Nilimuuliza Anitha aliyekuwa amesimama akiwa haamini kama amekutana na mimi "Anitha nani huyu.........?"Yule jamaa alimuuliza Anitha "Ni mpenzi wangu........."Anitha alijibu kwa sauti ya upole huku akiniangalia usoni,,,nilimuona mshkaji akiwa mpole ghafla "Bro samahani sana........"Mshkaji aliniambia huku akiniangalia usoni "Hakuniambia na wala sikujua kama ana mtu"Mshkaji aliniambia akionekana kunionea huruma sana "Naomba sana unisamehe bro,,nakuahidi sitaendelea tena kuwa na mahusiano na mwanamke huyu"Mshkaji aliongea kisha akageuza na kuondoka akimuacha Anitha amesimama akionekana kuwa na aibu sana "Inawezekana kabisa mi sio chaguo la moyo wako"Nilimwambia Anitha huku machozi yakinitoka "Inawezekana sifanani kuwa na wewe"Niliongea huku nikimuangalia Anitha aliyekuwa ameinamisha uso wake chini kwa aibu "Ni kawaida yangu kutafuta furaha ya moyo wako"Niliongea safari hii nikifuta machozi yaliyokuwa yakinitoka "Na ntaendelea kufanya hivyo kwa kukupa uhuru wa kufanya mambo yako"Niliongea huku nikihisi maumivu makali sana ndani ya moyo wangu "Endelea tu kufanya mambo yako ukimaliza tu utanitafuta,,mi nipo kwa ajil yako na siku zote ntaendelea kuwa #Body_Guard wa maisha yako"Niliongea huku nikianza kuondoka,,nilipiga hatua ya kwanza,,nikamaliza hatua ya pili macho yangu yakamuona Magreth akiwa na mwanaume mmoja mrefu mwenye mwili wa mazoezi "Aaaah Wilbat mamabo.........?"Magreth alinisalimia ka uchangamfu wa hali ya juu kiasi cha mi kumshangaa!! ************* Usikose Kusoma Namba Arobaini Na Mbili #Hakika_Kifo_Ni_Haki_Yangu Inaendelea Kupatikana,,Wahi Sasa Bado Hujachelewa Nawatakieni Usiku Mwema Wapendwa Wasomaji Wa Simulizi Zangu By #Hajrat
Posted on: Wed, 09 Oct 2013 16:44:55 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015