ZANZIBAR. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif - TopicsExpress



          

ZANZIBAR. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amewahimiza wananchi wa Zanzibar kuungana katika kulinda na kuhifadhi utamaduni, mila na silka za Wazanzibar, ili kuepusha tabia ya kuipotosha kwa makusudi inayofanywa na baadhi ya watu. Maalim Seif ameyasema hayo jana, wakati alipokuwa akihutubia katika hafla ya Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), yaliyoandaliwa na Madrasat Nur Islamiya huko katika kijiji cha Tumbatu Jongowe, Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja. Amesema utamaduni na mila za Wazanzibari ni za kipekee na zimerithiwa kwa miaka mingi, lakini baadhi ya watu wamekuwa na tabia ya kuvipotosha kwa malengo maalum, jambo ambalo linapaswa kupigwa vita na wananchi kulikataa. Amesema historia ya Zanzibar ina mafungamano makubwa na Dini ya Kiislamu kwa zaidi ya miaka 1000, hali ambayo inathibitishwa na kuwepo maeneo mengi ya kihistoria, ikiwemo msikiti wa Kizimkazi, magofu ya majengo ya asili huko Makutano katika kisiwa cha Tumbatu, pamoja na athari za iliyopo katika eneo la Kihistoria la Mkumbuu, kisiwani Pemba.
Posted on: Sat, 19 Oct 2013 07:14:58 +0000

Trending Topics



e="min-height:30px;">
#IfIHadAChurch Todays discussion is inspired by a fellow member
Cyndi enters and leads with a She-Bop (giving much of the audience
So, Found the missing iPhone, I HAD tossed it into the glove

Recently Viewed Topics




© 2015