hi admin,naitwa Sheila natokea mombasa ukonga nasoma chuo cha - TopicsExpress



          

hi admin,naitwa Sheila natokea mombasa ukonga nasoma chuo cha uhasibu. Nilikuwa natembea na mkaka mmoja ambae aliahidi kunioa kwani alionesha kila dalili na alikuwa akija nyumbani kama wazazi wangu wangeondoka,anakaa tunapiga stori afu baadae anaondoka. Kuna kipindi alikuwa akija home bila mm kujua na nakuja kushtuka yuko nyumbani ambapo nilimkanya kwa tabia hiyo kwani wazazi wangejua isingeleta picha nzuri na yeye alijitetea kwa kusema anajua muda ambao mama au baba anakuwaga hayupo nyumbani. Kwa kweli tumedumu kwa miezi tisa mpaka sasa. Ni hivi tarehe 10 ya mwezi huu,baba amemfukuza mdada wetu wa kazi kwani alipata ujauzito na alipohojiwa aliempachika hiyo mimba kamtaja boyfriend wangu,sikuamini kabisa,baba aliongozana na mdada wa kazi mpaka kwa huyo mkaka na wakamkuta ambapo alikiri na nyumbani wanawasiliana na nyumbani kwao na mdada wa kazi eti ndo afungishwe ndoa ya mkeka na boyfriend wangu,na hivi ndo maandalizi yashaanza,sijui mm nifanyeje kwani nikipiga simu ya huyo kaka haipatikani ingawa naambiwa yupo kwake. Naombeni mnishauri na mniongoze. Ahsanteni
Posted on: Tue, 27 Aug 2013 10:18:32 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015