ASEMAVYO SHABIKI WA MAN UNITED Natanguliza kile nilichokiona - TopicsExpress



          

ASEMAVYO SHABIKI WA MAN UNITED Natanguliza kile nilichokiona kisha nahukumu kwa kile ninachokiamini..Mpishi akipika vzr anaambiwa leo chakula kitamu, na akipika vibaya moja kwa moja anaambiwa ww sio mpishi jifunze kupika. Huwezi ukamuingiza Giggs, Welbeck na Smalling wakati una Kagawa, Chicharito na Zaha. Giggs anaingia namba 7 badala ya L.Nani, damu imara yenye skills inatoka inaingia damu nzito inayokaribia kuzeeka. South walikua wazuri kwenye kiungo, unamtoa Fellain unaingiza Welbeck kisha unamuita Giggs aje kati kupigana na wakina Wanyama kwenye kiungo. Haitoshi unamtoa Rooney unamuingiza Smalling kisha unamuambia Jones sogea pale kati ukamsaidie Giggs wakati ukijua Jones huyu huyu ndie alikua anajua mbio za Lambert zinaelekea wapi ili amkabe kirahisi. Sub 2 za kwanza zilikua kutojua ni mfumo gani autumie wa ushindi.. Sub ya mwisho ilijionesha dhahiri tumelizika na goal 1 na tunataka kuzuia kuondoka na point 3. Hii sio United ya kufunga goal 1 na kusubili dk 3 za mwisho kwa ajili ya kukaba. Pamoja na yote tunaweza kusema ni bahati mbaya ila lawama haziji bila kufanya makosa.. Mpira mbovu usio na muelekeo, kocha na benchi la ufundi mmeonesha kuingia darasani bila peni na kitabu. Kumbuka tuna mashabiki zaidi ya mil 350 duniani wanaowatazama na wanaohitaji kutuliza mioyo yao na nafsi zao.. Ni mawili, either benchi la ufundi libadilishwe lote au waje wachezaji wapya ambao wataendana na mfumo ambao kocha anautaka.
Posted on: Sun, 20 Oct 2013 01:15:01 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015