Babu kaenda kumtembeza mjukuu wake kwenye makaburi ya - TopicsExpress



          

Babu kaenda kumtembeza mjukuu wake kwenye makaburi ya kijiji; BABU: Unaona kaburi hili huyu jamaa alikuwa mtu, nilimkopesha fedha, akajitahidi sana kunilipa, kwa bahati mbaya alikufa huku namdai alfu hamsini. Nina uhakika huyu kaenda mbinguni alikuwa mtu mzuri sana.........wa kaenda kaburi jingine BABU: Sasa huyu alikuwa mshenzi sana alikopa laki yangu hakunilipa makusudi mpaka akafa na deni langu. Huyu lazima yuko motoni MJUKUU: Dah babu ukifa una bahati kweli BABU: Una maana gani na wewe? MJUKUU: Yaani babu ukifa ukienda mbinguni kuna hela zako, ukienda motoni kuna hela zako BABU: Mjinga mkubwa twende nyumbani
Posted on: Thu, 15 Aug 2013 19:30:52 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015