Cairo Kiongozi aliyeondolewa madarakani wa Misri Muhammad Mursi - TopicsExpress



          

Cairo Kiongozi aliyeondolewa madarakani wa Misri Muhammad Mursi amesema kuwa alitekwa nyara na kikosi cha Republican Guard kabla ya mapinduzi yaliyomuondoa madarakani Julai mwaka huu. Mursi amesema katika barua iliyosomwa jana kwenye televisheni na wakili wake Mohamed Damati kwamba, Wamisri wanapaswa kutambua kuwa alitekwa nyara na kupelekwa katika kituo cha Republican Guard kwa siku kadhaa na baadaye alihamishiwa katika kituo cha jeshi anakoshikiliwa kwa miezi minne. Muhammad Mursi amesisitiza kuwa yeye ni rais halali wa Misri na kwamba ameondolewa madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi. Amesema Misri haitapata amani hadi pale mapinduzi hayo yatakapokomeshwa na wahusika wote kuchukuliwa hatua za kisheria. Zaidi ya watu 1000 wameuawa katika machafuko yanayohusisha jeshi la Misri na wafuasi wa Muhammad Mursi wanaotaka kiongozi huyo arudishwe madarakani. Source Tehran Swahili
Posted on: Fri, 15 Nov 2013 09:53:07 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015