Daah nimevaa pensi yangu ya turubai na chupi langu la chadema nipo - TopicsExpress



          

Daah nimevaa pensi yangu ya turubai na chupi langu la chadema nipo kifua wazi nimeingia bafuni kuoga Ile nimevua tu pensi naitundika kene msumari nikasikia simu yangu ya kichina inaita kwenye mfuko wa pensi kuangalia nakuta ni demu mmoja hivi mkali balaa tunakaa naye pale kitaa kila nikimtongozaga ananizingua ananikataa nimefurahi sana kuona yeye ndo ananipigia nimerukaruka sana mule bafuni nikajua atakuwa amejifikiria anataka kunipa jibu zuri nilivyopokea akaniuliza "cox dear uko wapi?? Nikamjibu "niko nyumbani mrembo" akaniambia "fanya fasta washa redio usikilize Radio free" nikamuuliza "kuna nini bby?? Akaniambia "we sikiliza fasta kuna bonge la suprise nimekufanyia mda huu" nimetoka bafuni fasta huku nimevaa chupi langu la chadema nna mapovu ya sabuni usoni nimekimbia ndani kuwasha redio nikajua labda mrembo atakuwa amenitumia salamu za mapenzi au kutakuwa kuna kanyimbo kazuri ka mapenzi amenidedicate Nimeweka redio free nimeshangaa nakuta kuna matangazo ya vifo nguvu zote zimeniishia nimekasirika vibaya mno nikampigia simu nikamuuliza "mrembo mbna nimeweka redio free nimekuta matangazo ya vifo??? Akaniambia "sasa wewe ulitaka ukute nn mm nilikuwa nakupima tu na lichogo lako nione kiherehere chako" nikamwambia "sio vizuri mrembo mm nilijua umenitumia salamu za mapenzi au kuna kanyimbo ka mapenzi unataka nikasikilize" akacheka kwa dharau akaniambia "we mbulula kweli yani mm nikutumie salamu za mapenzi chogo kwa kipi ulichonacho tena ukome kunisumbua na kuja kuja nyumbani ovyo nasikia jana ulikuja hapa na likofia lako la mkeka mwisho leo nisikuone tena unajipitisha hapa nyumbani" Daah roho imeniuma sana yani mimi nimetoka bafuni na chupi tu na mapovu usoni nikajua naenda kusikiliza kitu kizuri kwenye redio kumbe majanga nakutana na matangazo ya vifo na kutukanwa na demu juu nimelia sana hata hamu ya kuoga sina tena GONGA LIKE/SHARE/KAMA UMEIPENDA HII STORY
Posted on: Sat, 05 Oct 2013 06:44:48 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015