Fursa ya kupata commission na tovuti ya Maskani Hii fursa iko - TopicsExpress



          

Fursa ya kupata commission na tovuti ya Maskani Hii fursa iko wazi kwa kila raia wa Africa Mashariki ambaye anaweza kupiga picha za matukio na maeneo yaliyopo kwenye wilaya yake anayoishi na kuweka kwenye tovuti yetu katika mkoa wake angalau mara mbili kwa wiki. Haihitaji uwe na utaalam wa aina yoyote ili mradi uwe na simu ya mkononi inayoweza kupiga picha na kuweza kuweka maelezo ya picha hiyo ama kwa Kiingereza au Kiswahili kwa nchi za Tanzania na Kenya, Kiingereza kwa Uganda na Kifaransa au Kingereza kwa nchi za Rwanda na Burundi. Kitu chochote kile ndani ya wilaya yako unaweza kukipiga picha na kukiwekea maelezo kidogo kama vile accidents, traffic jam, mazao, ziwa, mito, milima, matengenezo ya barabara, vituo vya mabasi, shule, vyuo, viwanja vya burudani, wajasiriamali, wasanii, sanaa, wanasiasa, wachezaji, alama za utamaduni wa kabila au makabila yaliyomo wilayani kwako, maduka, ofisi za Serikali, migahawa, hoteli, nyumba za kulala wageni, vituo vya Taxi, vivutio vya utalii, maeneo ya burudani, party, mziki, ngoma za kienyeji, wanyama, ndege, sehemu maarufu, mikutano ya siasa, sehemu za mapumziko, n.k. Tunahitaji watu 50 kutoka kila wilaya iliyopo ndani ya Africa Mashariki. Tutato fursa hizi kwa awamu. Awamu ya kwanza itaanza na mpiga picha mmoja kwa kila wilaya. 20% ya hela ya mauzo yatakayopatikana ndani ya tovuti ya Maskani yatagawanywa sawa sawa kwa wapiga picha wote wa maskani. Wapiga picha Waanzilishi wa Maskani watapata haki ya kupata 10% ya hela itakayopatikana kwa wapiga picha watakaochukua nafasi zao milele kama watadumu na Maskani kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja. Kwa watakaohitaji kujumuika nasi kwenye fursa hii, wasiliana nasi kupitia email hii info@maskaniyetu Maskani, tovuti pekee inayoangaza Africa Mashariki kuanzia ngazi ya wilaya maskaniyetu
Posted on: Mon, 30 Sep 2013 13:36:46 +0000

Recently Viewed Topics




© 2015