HII NDO NAFASI YA KISWAHILI DUNIANI. Kiswahili inaaminika kuwa - TopicsExpress



          

HII NDO NAFASI YA KISWAHILI DUNIANI. Kiswahili inaaminika kuwa lugha asili ya Afrika inayozungumzwa na watu wengi kusini mwa jangwa la sahara. Kama tunavyojua, ni lugha ya taifa kwa nchi za Tanzania na Kenya, na pia yazungumzwa kwenye nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi, Rwanda, Uganda na visiwa vya Comoro. Kiswahili ndio lugha pekee ya kiAfrika iliyo miongoni mwa lugha rasmi za Umoja wa Afrika. Na inaaminika kuwa lugha ya saba kwa watumiaji wengi duniani Na matumizi yake kama lugha inayozungumzwa na wengi wenye lugha tofauti katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati unaifanya lugha hii kuwa muhimu zaidi kwa watu wengi walio na mahusiano na / ama wanaotaka kujishughulisha na biashara, kazi ama diplomasia katika ukanda huo. Kiswahili sasa kinafunzwa katika vyuo 3 hapa Misri, na vyuo visivyopungua 50 nchini Marekani, lakini pia inafundishwa kwenye vyuo vikuu mbalimbali Ulaya na hata bara Asia. Kiswahili ni lugha muhimu katika habari, shule, kazi za kiofisi, kidiplomasia na hata usalama miongoni mwa mataifa na naamini ndio sababu hata Markazi ya Watanzania hapa Misri, wakaona ni jambo la busara kuanzisha darasa la kufunza Kiswahili kwa watu wa mataifa mbalimbali na wenji hapa Misri.
Posted on: Thu, 17 Oct 2013 18:33:54 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015