Huenda mgomo uliopangwa kuandaliwa na Walimu kote nchini ukapata - TopicsExpress



          

Huenda mgomo uliopangwa kuandaliwa na Walimu kote nchini ukapata suluhu ya kudumu baada ya kamati ya bunge kujadiliana kuhusu swala hilo na kuamua kupunguza shilingi bilioni 4 kutoka kwa bajeti iliyotolewa awali.Fedha hizo zimepunguzwa kutoka kwa Wizara za Utalii na Viwanda zilizopunguziwa bajeti zao kwa shilingi bilioni 2 kwa kila wizara ili kuweza kusuluhisha matakwa ya Walimu.Kamati hiyo pia ilipinga bajeti ya shilingi milioni 700 za ujenzi wa ofisi ya Rais mstaafu Mwai Kibaki na kuapa kuipunguza ili kuweza kusimamia matakwa ya walimu huku kamati hio pia ikiitaka kamati inayosimamia sekta ya elimu kujadiliana tena kuhusu shilingi milioni 17 zilizotengewa ununuzi wa vipatakilishi wakiutaja mradi huo kutokuwa na umuhimu iwapo Walimu watakuwa hawajatekelezewa Matakwa yao.Je unadhani hatua hii ya Kamati ya Bunge ni suluhu mwafaka kwa tatizo hili la Walimu?Voroni ukiwa na Dama na Kalambua.
Posted on: Wed, 19 Jun 2013 03:22:13 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015