Huu ndio wakati ambao vyuo vingi kuna Mahafali - TopicsExpress



          

Huu ndio wakati ambao vyuo vingi kuna Mahafali Mfululizo(Graduation), sasa kama una Mpenzi wako wa chuo kahitimu basi usikurupuke kubelea maua na mataji na kujitia upo front line na Ma-hug kibao,ohooo utakuja kuaibika bureee,CHUNGUZA KWANZA MAANA KULE CHUO UONGO MWINGI!!!! Pale kwenye GRADUATION ndio sometimes huleta uhalisia wa mambo!, nakuapia hakuna mhitimu atakayeruhusu Bwana au Bibi yake wa kuzugia kule Chuoni ajitie shobo na kimbele mbele kwa wazazi! Yaani wale walioficha pete za ndoa kwenye mabegi kule chuo hakika siku hiyo watazivaa na wanandoa wenzao watakuwepo kuwapongeza! Na kama ndio mrembo matata njoo umuone jamaa yako wa tangu semister ya kwanza ambaye aliahidi kukuoa! huwezi amini siku hii mkewe na watoto saba wametoka Biharamuro kuja kwenye Graduation ya Baba! sasa na kama wewe ni kidume uliyeliwa viji-hela vyako vya Bumu za Loan Board utakaa umekodoa macho mpaka michozi! >>>Mwenzenu mwaka jana nilijitia kimbelembele kwenye Graduation ya Kipenzi changu pale IFM nikajikuta nimezubaa tu na maputo yangu hakuna hata anayenijali, yaani siku hiyo nilibebelea maua utadhani Mfanyakazi wa Bustani ya Wahindi kule Lushoto!, Baadae nikashangaa Jamaa mmoja mwenye kipara kavaa Panjabi kamkamatia kiuno Kipenzi changu huku anabusu tu Joho! daaah!,
Posted on: Wed, 23 Oct 2013 09:32:36 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015