Ifuatayo ni Historia fupi wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius - TopicsExpress



          

Ifuatayo ni Historia fupi wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.... Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa raisi wa kwanza wa Tanzania, alizaliwa Butiama mkoani Mara mnamo tarehe 13 April 1922 na alifariki dunia 14 Oktoba 1999. Alikuwa mojawapo kati watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki. Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya babake; katika umri wa miaka 12 aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi Musoma. Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea kusom a shule ya wamisionari Wakatoliki huko Tabora. Katika umri wa miaka 20 alibatizwa akawa mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake. (Mama Maria Nyerere, mke wa Hayati baba wa Taifa) Mapadre wakaona akili yake wakamsaidia kusoma ualimu huko Makerere, Kampala, Uganda kuanzia 1943 - 1945. Makerere akaanzisha tawi la Umoja wa wanafunzi Watanganyika pia amejihusisha na tawi la Tanganyika African Association (TAA). Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi Tabora akifundisha shule ya St.Mary´s. Mwaka 1949 alipata skolashipu ya kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh huko Uskoti / Uingereza akasoma M.A. ya historia na uchumi(alikuwa mtanzania wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na mtanzania wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya Tanzania). Aliporejea Tanganyika kutoka masomoni, Nyerere alifundisha Historia, Kingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam. Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa raisi wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), cham a ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Makerere. Mwaka 1954 alikibadilisha chama cha TAA kwenda katika chama cha Tanganyika African National Union (TANU) ambacho kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kilikuwa tayari chama cha siasa kinachoongoza Tanganyika. Uwezo wa mwl. Nyerere uliwashitua uongozi wa kikoloni na kumlazimisha Nyerere kuchagua kati ya siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akisema kuwa alikuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya. Alijiuzuru ualimu na kuzunguka nchini Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta muungano katika mapigano ya uhuru. Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Trusteeship council na Fourth committee ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York. Uwezo wake wa kimaongezi na kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu. Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo bwana Richard Turnbull ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru. Nyerere aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1960. Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake na tarehe 9/12/1961 Nyerere alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Tanganyika huru na mwaka mmoja baadae Nyerere alikuwa raisi wa kwanza wa jamhuri ya Tanganyika. Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania baada ya mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah. Sifa zake Bado anakumbukwa na watanzania hasa wa hali ya chini kutokana na sera zake za kujali utu na ubinadamu.Pia ataendelea kukumbukwa na waafrika kote barani hasa kwa mchango wake mkubwa wakati wa harakati za kupigania uhuru katika nchi mbali mbali barani Afrika. Ni mmoja wa viongozi wachache wanaokumbukwa kwa kutojilimbikizia mali pamoja na kutawala kwa miaka zaidi ya 24. Mwishoni mwa maisha yake Nyerere aliishi kama mkulima wa kawaida kijijini kwake Butiama. Alipatwa na kansa ya damu (leukemia) na kufariki Uingereza wakati wa kutibiwa katika mji wa London tarehe 14 Oktoba, 1999. Alizikwa mahali pa kuzaliwa kwake, kijiji cha Butiama. (Kaburi la Baba wa Taifa) Watanzania tumempoteza kiongozi mpiganaji na mwenye uchungu na nchi yake, aliepinga vita dhidi ya umasikini, ubaguzi na rushwa. Hamna kiongozi mwengine alieiga mfano wa Baba wa Taifa tumebakiwa na viongozi wenye uchu na madaraka kujirumbukizia mali wao na familia zako ni aibu sana kwa Taifa maana enzi za Mwalimu hapakukuwa na hali hii ya kiongozi kumiliki mali nyingi mfano mzuri alionesha yeye ambae hakuwa na uchu wa kujirumbikizia mali ingawa alikuwa na nafasi kubwa na inayomfanya aweze kufanya hivyo lakini alikuwa na uzalendo na nchi yake. Nchi sasa inapoteza dira hamna viongozi bora ila kuna bora viongozi aibu kwa Watanzania. 1.Nyerere enzi za uhai wake picha namba moja 2.mke wa Nyerere mama Maria Nyerere 3.Nyerere enzi za Uhai wake akiwa katika maisha ya kawaida 4.Kaburi la Baba wa Taifa .Pumzika kwa Amani Baba amaa kweli kazi ulichapa kwa Moyo Tulikupemda likini Mungu zaidi yetu Bwana alitoa na pia alitwaa jina lake lihimidiwe Amina .
Posted on: Mon, 14 Oct 2013 05:41:33 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015