JE INAJUZU TAASISI YA KIDINI KUSAJILIWA NA SERIKALI ZA - TopicsExpress



          

JE INAJUZU TAASISI YA KIDINI KUSAJILIWA NA SERIKALI ZA KIKAFIRI? Kabla ya kujibu swali hili kuna mambo kadhaa yafaa kufafanuliwa ili iweze kuwa wazi: Kwanza, katika sheria za kikafiri Waislamu wanaangukia moja katika sehemu tatu katika kudai haki zao: a. Kulazimishwa kufanya au kufuata kwa khiyari mambo ambayo Uislamu unayakanusha na kuyapinga kama zinaa, kamari, rushwa, kupiga kura kuwachagua watawala watakaotawala kwa mujibu wa sheria za kikafiri nk. HUKUMU YA MAMBO HAYO NI KUJIEPUSHA TU. b.Kuna haki ambazo Uislamu umezitambua ni haki zako au wajibu wako, lakini makafiri wamezikanusha hizi katu huwezi kuzipata kwa makafiri. Mfano ni haki yako ukiiba ukatwe mkono pia ni haki yako ukizini upate bakora au upigwe mawe, haki hizi tamu na adhiimu. Lakini makafiri hawakupi na hawaruhusu mtu yeyote akupatie haki kama hizi. Ni jukumu kuongeza bidii ya kutafuta serikali ya Kiislamu ili zipatikene. c. Haki ambazo asili Uislamu umekupa na unakuruhusu bali ni wajibu kufanya mambo haya utayafanya tu, hata kama serikali hizi zitapinga na kukataa. Mfano kusali, kufunga kuhiji, kubeba dawa, kuasisi taasisi ya Kiislamu yenye masharti ya Kiislamu nk, Hapa ndipo penye utata na InshaAllah tutafafanua. Kwa mfano, serekali ya Tanzania inaruhusu watu kwenda Hijja, na wanaotaka kwenda Hijja kuna utaratibu wa kwende kuomba kibali kama viza, passport nk. Kwenda kuomba viza si haramu kwani unataka kwenda hijja, na Uislamu umekubali hijja. Na pia hawa makafiri wamekubali hija. Hivyo, kuenda kutaka vibali vya hija si haramu kwani Uislamu umeitambua ibada ya hijja. Na hapa tutatoa dalili ya Mtume SAAW na maswahaba. Lakini ifahamie kuwa kwenda kwetu kule si kukiri na kuridhikana masharti yao hayo. Bali ni kuwa Uislamu umekuruhusu tu, na lau kama watakataa kutoa kibali lazima ufanye kwa nguvu na litakalokuwa na liwe. Yaani Uislamu una taka kama unaweza kutekeleza Uislamu wako bila madhara tekeleza. Lakini ikiwa huwezi kutekeleza Uislamu basi madhara yafanyike lakini Uislamu utekelezeke. Hivyo, lau hijja izuiliwe Waislamu hulazimika waenda kwa njia yoyote hata ya kupenya mipakani kwa siri au usiku kwa maboti, njia za panya nk. Mtume swalallahu alaihi wasalama aliporudi Makka kutoka Taif alikataliwa kuingia Makka. Ilhali Uislamu unampa haki Mtume SAAW ya kuingia Makka na makafiri wanaitambuwa haki hiyo hata kwa mujibu wa sheria zao. Mtume SAAW ana haki ya kuingia Makka ila tu pakahitajika mdhamini ili Mtume SAAW aingie. Basi Mtume SAAW akaenda kwa Mutim bin Adiy na kuchukua dhamana ya Mtume SAAW kuingia Makka. Hivyo ndivyo ilivyo Muislam lazima abebe daawa lakini ikiwa makafiri wanataka upeleke taarifa ili wakupe makaratasi ya wewe kufanya daawa. Si haramu kwenda lakini endapo watakataa ni lazima uendelee na daawa yako. Amma dalili ya pili ni kuwa Abuu bakr Swidiqi alipokwenda kuomba ruhusa na dhamana ya kuswali nje ya nyumba yake baada ya makafiri kuwapiga marufuku Waislamu ndani ya Makka wasiswali nje. Abuubakri alikwenda kwa kafiri akachukua dhamana ili aswali nje mbele ya nyumba yake. Makafiri walipo mfata kutaka kumzuia akawaambia nina dhamana ya mtu fulani wakamuacha na kuendelea kufanya ibada nje ya nyumba yake kwa sauti. Makuraishi wakaona badoAbu bakar anawaathiri wafuasi wao hivyo wakataka dhamana ile ifutwe na Abuu bakar aadhibiwe kwa kuswali nje ya nyumba yake. Yule mtu aliyemchukulia dhamana Abuu bakar akakataa kata kata kuondosha dhamana yake. Lakini Abuu bakri akaona isiwe tabu akajiondosha katika dhamana ya yule mdhamini na akaendelea kuswali nje ya nyumba yake. Mara tu baada ya dhamana ile kuvunjwa makuraish wakaja kumpiga sana Abu bakar kiasi cha kushindwa kutofautisha kati ya komo na chogo. Hapa tunapata dalili ya kumbe kupeleka taarifa kwa makafiri kuwa unataka kufanya jambo fulani si haramu, lakini lau wanakataa wewe lazima uendelee kufanya ibada hiyo. Kwa hivyo kusajili taasisi au chama cha kidini asili si haramu. Kwani ni kama kupeleka taarifa tu kuwa unataka kufanya kitu fulani lakini lau kama watakataa basi lazima kazi ile uifanye tu hata kama utapata kipigo. Na hivi ndivyo ilivyo fanya Hizb mwanzoni muasisi wake wa kwanza alipeleka taarifa kwa watawala wa Mashariki ya Kati licha ya wao kukataa lakini kazi iliendelea kama kawaida. Sasa upelekaji taarifa kama huu utaitwa leseni, ruhusa, usajili, taarifa nk. Si hoja msingi muhimu. Kilicho muhimu ni mawasiliano ya aina hiyo kati ya taasisi ya Kiislam, mtu au kundikwa upande mmoja na serikali za kikafiri kwa upande wa pili. TANBIHI: 1. Tawala hizi za kikafiri si yooote wayafanyao ni haramu. Bali msingi wao ndio kufuru lakini yapo mambo wayafanyao si haramu. Mfano kujenga bara bara nk si haramu wala huwezi sema barabara hii siikanyagi kwa sababu imejengwa na maakafiri. Aidha, baadhi ya kanuni zao zipo ambazo hazigongani na Uislamu. Kanuni kama hizo ni halali kuzitumia lakini kwa sharti wakati unazitumia, tumia kwa kuwa Uislamu umehalalisha na si kuwa makafiri wamehalalisha. Je kuna dalili ya hilo? Ndio, hija ya makuraishi kabla ya Uislamu waliitia vitimbi na vituko. Baada ya kuja Uislamu baadhi ya maswahaba wakaona tabu kuhiji na kufanya baadhi ya matendo kama yaleeee ya kijahiliya. Uislamu ukaja ukaleta sheria mpyaa si zile za makuraishi lakini zikafanana na za makuraish na wakaambiwa fanyeni hivyo. Kufanana baadhi ya sheria za Kiislamu na za makafiri si kikwazo bali tutazifanya tu. Basi na kadhia ya usajili ni kama hali hii. 2. Sheria ya Kiislamu inaruhusu mtu kuasisi chama, taasisi, kundi, tv, redio, gazeti nk. Bila ya kutanguliza maombi ya ruhusa ila ukisha asisi basi taarifa iende kwenye dola ya Kiislamu. Hivyo leo kuna serikali hizi za kikafiri zina makundi mawili kundi la kwanza mafuruku kuanzisha mpaka uombe ruhusua na kundi la pili anzisha kisha peleka taarifa. Hivi ndivyo ilivyokuwa nchi kama Lebanon, Tunis,Jordan nk. Hata wabunge binafsi zama za nyuma walikuwa wana ruhusiwa yaani unaingia bungeni bila sharti lolote la serikali wala kudandia chama chochote. 3.Hizb imeshapeleka taarifa kwa serikali kadhaa kuwa ipo na inafanya kazi hivyo baadhi zikakurupuka na kutangaza kuipiga marufuku kama Jordan nk. na hizb haikusita na harakati zake, baadhi zikakaa kimya, na baadhi zikajibu kukubali kama Lebanon na Tunis. Lakini si kukubali kwa ridhaa kwani walijibu kukubali huku wanaendelea kuwakamata na kuwatesa mashabau wa hizb. Suala hapa ni kuwa hizb inapeleka taarifa huku kazi zake zinaendelelea kama kakwaida kabla ya majibu au baada ya majibu. Na amma majibu yakiwa ni kukubaliwa au la. Hayo si kikwazo kwetu. 4) Ikiwa masharti ya nchi ya unayoasisi jumuiya ni mabovu na yanakhalifu Uislamu moja kwa moja haina haja kwenda kupeleka taarifa. Mfano, Tanzania kuwa wao sharti lao msingi ni kwamba chama au taasisi ikijihusisha na dini basi ijiepushe na siasa. Na kama ni ya kisiasa ijiepushe na dini. Hii kanuni ipo wazi kutofaa kwake basi huwa ni haramu kwenda kusajili chama cha dini kwa kufata masharti ya haramu kama kukubali kuasisi taasisi isiyojihusisha na siasa. Sharti hilo ni haramu kukubali na Kwa kuhitimisha hapa ndipo kwenye nukta nzito watu wazingatie kunaposemwa na baadhi ya watu kuwa ni haramu kusajili taasisi ya kidini huwa msingi wao ni huo wa masharti kukhalifu Uislamu. Kwa kuwa hutarajiwa masharti ya usajili wa nchi nyingi yanakahalifu Uislamu kwani yanataka ukiri kufanya kazi nusu ya dini na nusu ya pili uachane nayo. Hivyo wengi wameishia kusikia uharamu wa kusajili taasisi ya dini bila kusikia muendelezo wa sentesi ya pili ya uharamu huu. Kwa hivyo, Hizb imefanya kama alivyofanya Mtume SAAW na Swidiq yaani kutoa taarifa ili kuepusha shari zao zisizokuwa za lazima. Lakini lau dola hizo wakikataa kazi inaendelea huku msingi wa Uislamu ukichungwa wa kutotenganisha dini na siasa au siasa na dini. Nawasilisha nasubiri maswali kisha tutaendelea. Naomba hoja za kidini. Huu ufafanuzi ni hukmu ya kisheria.
Posted on: Sun, 25 Aug 2013 17:24:20 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015