KATIKA ITV ALHAMISI 28/11/2013 12:30 USIKU Fuatilia - TopicsExpress



          

KATIKA ITV ALHAMISI 28/11/2013 12:30 USIKU Fuatilia mfululizo wa vipindi maalum vya SOKO LA HISA NA MITAJI –DSE katika kuelimisha umma, taasisi na asasi mbalimbali umuhimu wa kujiunga na mfuko huo kwa manufaa yao na vizazi vijavyo. 1:00 USIKU Usikose kuangalia kipindi cha UZALENDO kikihusu mambo yanayojili katika medani ya siasa nchini. Leo ni Mh. Felix Mkosamali Mbunge wa Muhambwe NCCR Mageuzi na Mh. Suzan Kiwanga Mbunge Viti Maalum Chadema wakijadili uwepo wa wabunge wa vyama vya upinzani bungeni. Je, wana tija au ni mzigo? 1:30 USIKU Lean Cooper ataka kuhakikishiwa usalama wa maisha yake ili atoe kidhibiti cha kukamatwa kwa Anthony Lamberti aliyewateka Calvin na Prada na kuwapa kichapo. Na Zeb Matabani aelezwa kuwa mvumilivu kuhusu hali ya mkewe. Hii ni tamthilia ya kusisimua ya ISIDINGO THE NEED. 3:00 USIKU Katika MALUMBANO YA HOJA, fuatilia mada ya leo isemayo Migogoro ya ndani ya vyama vya siasa. Je, ni kukua kwa demokrasia? Kipindi kitawajia mojakwamoja kutoka studio na ushiriki wenu ni muhimu mno. 5:30 USIKU Fuatilia kipindi maalum cha TUSKER PROJECT FAME kinachokujia kila siku kikionyesha shughuli zinazofanywa na wasanii kwa kila siku. KWA MAONI NA USHAURI USISITE KUTUANDIKIA [email protected] ------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Posted on: Thu, 28 Nov 2013 06:42:57 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015