KATILI WA WANAUME. Sehem ya 9 ILIPOISHIA:Kwa kweli maisha ya - TopicsExpress



          

KATILI WA WANAUME. Sehem ya 9 ILIPOISHIA:Kwa kweli maisha ya kijijini na mjini yana tofauti kubwa, maisha niliyokuwa nikiishi Lindi yalikuwa na tofauti kubwa kwa kila kitu. Nilipendeza mtoto wa kike ungekuja haraka ungenipotea.Nywele nilikuwa nimezitia dawa na kupendeza hata mavazi yangu yalikuwa ya bei mbaya. Mose alininunulia na simu ya bei mbaya, nami sikuwa mwizi wa fadhila nilichokipata toka kwa Mose nilimpa dada. NA zingine nilizituma nyumbani kwa ajili ya wanangu na wazazi wangu. Siku zote Mose aliniomba tuoane baada ya familia yao kuridhika na mimi. Nilikuwa nikimrusha mpaka ikafikia mwaka na hamu kubwa ya Mose ni mtoto na mtoto alimtaka ndani ya ndoa. Japo nilikuwa na wasiwasi wa kuolewa huenda Mose akakutwa na mauti, lakini wasiwasi wangu niliuondoa baada ya kukaa na Mose zaidi ya mwaka na nusu bila tatizo lolote kitu ambacho mwanzoni hakikuwahi kutokea. Nilijifikiria kama ningekubaliana kuzaa na Mose muda ule ningekuwa tayari nimeisha jifungua mtoto wa mwezi mmoja. Kila kukicha Mose aliniomba nikubali tufunge ndoa ili tuishi katika ndoa ya halali. Hakuwa yeye tu wazazi na ndugu zake nao walivutiwa na tabia yangu ambayo kila mmoja alitaka niolewe. Si hao tu dada binamu na shemeji nao walikuwa mstari wa mbele kunibembeleza niolewe na Mose. Uamuzi wa kukubali kuolewa ulichukua nusu mwaka ikiwa nimetimiza muda wa mwaka na nusu namzungusha Mose. Sikuwa na jinsi nilikubali kuolewa na Mose kitu kilicholeta furaha kwa pande zote za familia. Kutokana na uwezo wa Mose kifedha wazazi wangu nao toka nyumbani Lindi walihudhuria harusi ya kwanza ya aina yake katika maisha yangu. Bado niliendelea kuamini maisha ya kijijini na mjini yana tofauti kubwa. Ilikuwa harusi ambayo katika maisha yangu niliiona kwenye sinema na si kitu live. Mariamu mimi nilikuwa kama malaika jinsi nilivyopendeza, kila mmoja ukumbini alinisifia jinsi nilivyopendeza. Harusi ilikwisha salama kila mtu ikibakia simulizi mdomoni mwake tukawa simulizi si katika kupendeza kwa maharusi tu, ukumbi chakula na vinywaji kwa watu kula na kunywa mpaka kusaza. Nilimshukuru Mungu harusi yangu iliisha salama nami kuyaanza maisha ya kuwa mke wa mtu mwenye hadhi ndani ya familia. Kwa kweli hakuna kilichopungua kwangu zaidi ya kuongeza upendo kwa wote. Siyo siri ndani ya mwezi mmoja nilipendeza na kunawiri mara dufu, kwa kweli ndoa ilinipenda nami kwa mara ya kwanza nilijiona ni kiumbe niliyezaliwa upya kuolewa na bwana mwenye uwezo pia mwenye upendo wa kweli kwa kuweza kunivumilia zaidi ya mwaka na nusu. Nami niliuapia moyo wangu kumpa penzi la kweli na kujitoa muhanga kwa ajili yake, kuhakikisha nampa kile alichokitafuta zaidi ya mwaka na nusu. Siyo kwamba kipindi cha mwaka na nusu hatukuwa na uhusiano wa kimapenzi. Tulikuwa nayo ila tulitumia kinga kila tulipokutana ili kusubiri muda wa kuoana tuweze kupata mtoto wa halali wa ndani ya ndoa. Si mimi hata mume wangu ndoa ilimfanya anawiri na kupendeza machoni mwa watu. Mmh! Jamani ndoa nzuri hasa umpate akupendae kwa dhati. Utafikiri ilikuwa ikisubiri ile kugusa mtoto wa kike nikanasa. Nilipomueleza hali yangu mume wangu kuwa nimenasa alifurahi na kusema: “Unaona mke wangu bila kuwa waangalifu ujauzito huu ungeingia nje ya ndoa.” “Ni kweli unaonekana una mbegu kali,” nilimsifia mume wangu. “Kwa mwanaume yeyote aliyekamilika na mwanamke aliyekamilika wakikutana lazima hali hii itokee labda pawepo matatizo.” “Mmh! Kweli, mume wangu unapenda mtoto gani?” “Yeyote tutakaye jaliwa na Mungu siwezi kumpangia.” Itaendelea towa ushirikiano kwa #LIKE & #SHARE
Posted on: Sat, 26 Oct 2013 13:49:47 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015