KITI CHA MBUNGE WA DENMARK SHS LAKI. NNE(400,000), KITI CHA MBUNGE - TopicsExpress



          

KITI CHA MBUNGE WA DENMARK SHS LAKI. NNE(400,000), KITI CHA MBUNGE WA TANZANIA SHS MILIONI TATU(3,000,000) Jana tumetembelea bunge la Denmark, wao wana wabunge 170 tu na viti vyao kila kimoja ni dola 250 ambazo ni sawa na shilingi LAKI NNE NA NUSU za Tanzania. Viti vyao ni vya kawaida sana, si viti ghali, kiti kimoja cha mbunge wa Tanzania ni zaidi ya Dola elfu moja mia saba ambazo ni zaidi ya shilingi milioni tatu za Tanzania na ni ghali mno mara sita ya kiti cha mbunge wa Denmark. Kichekesho ni kuwa, bajeti ya Tanzania ni trilioni takribani ishirini(20) kwa mwaka huku bajeti ya Denmark ni takribani trilioni mia tano (500)kwa mwaka. Wao wana bajeti kubwa na wana matumizi ya kawaida. Sie tuna bajeti ndogo na tuna matumizi makubwa. Mwenye trilioni mia tano ananunua kiti cha mbunge kwa shilingi laki nne huku mwenye trilioni ishirini ananunua kiti cha mbunge cha shilingi milioni tatu. Mara kadhaa CUF imesisitiza kuwa, lazima Tanzania itafute serikali ambayo itabana matumizi kwa vitendo. Tanzania ikitumia vyanzo vya sasa vya mapato tunaweza kubadili uchumi wa nchi yetu kabla hata hatujavuna dhahabu na gesi wala kusubiri misaada ya wazungu
Posted on: Thu, 21 Nov 2013 16:02:23 +0000

Trending Topics



="sttext" style="margin-left:0px; min-height:30px;"> Immediately Prof.Kodandaram has to give a statement if any
Living in dependence on Me is a glorious adventure. Most people
Kingsley Anayo Ojimadu: Some call it unwanted pregnancy and

Recently Viewed Topics




© 2015