Katika Ngazi Za Kimataifa, Kocha Wa Bayern Munich Pep Guardiola - TopicsExpress



          

Katika Ngazi Za Kimataifa, Kocha Wa Bayern Munich Pep Guardiola Amejitokeza Na Kupinga Habari Zilizoenea Kuhusu Hatua Ya Klabu Yake Kutaka Kumsajili Beki Wa Chelsea David Luiz. Ilikisiwa Kuwa Kocha Huyo Alikuwa Tayari Kutoa Kima Cha Pauni Milioni Arobaini Ili Kupata Huduma Za Mchezaji Huyo. Aidha Kocha Huyo Ameeleza Kuwa Ana Wachezaji Wa Kutosha Msimu Ujao Hivyo Basi Hana Haja Kumsajili Luiz. Hayo Yakiarifiwa Mkufunzi Wa Manchester United David Moyes Amewasili Nchini Uingereza Kusuluhisha Matatizo Yanayomkumba Na Mshambulizi Wayne Roney. Kocha Huyo Anatarajia Kufanya Mazungumzo Na Rooney Ili Kumhakikishia Kuwa Atakuwa Kiungo Muhimu Katika Klabu Hiyo Msimu Ujao. Kwingineko Totenham Inapanga Kujiunga Na Arsenal Kwenye Harakati Ya Kumsaka Luiz Suarez Kuchukua Nafasi Yake Gareth Bale Ambaye Anatarajiwa Kujiunga Na Real Madrid Iwapo Klabu Hiyo Ya Uispania Itamudu Matakwa Ya Spurs. Uhamisho Wa Suarez Kutoka Liverpool Umekuwa Kizungumkuti Kwani The Reds Wanadai Kima Cha Pauni Milioni Hamsini, Bei Ambayo Arsen Wenger Hayuko Tayari Kutoa. Hata Hivyo, Endapo Real Madrid Itakubali Kumnunua Bale Kwa Kitita Cha Pauni Milioni Themanini Na Tano Kama Ilivyo Matakwa Ya Totenharm, Klabu Hiyo Ya Uingereza Itakuwa Katika Nafasi Bora Ya Kumsajili Suarez.
Posted on: Wed, 31 Jul 2013 10:19:37 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015