Kitendo cha Moyes kumteua R. Giggs kuwa kocha mchezaji - TopicsExpress



          

Kitendo cha Moyes kumteua R. Giggs kuwa kocha mchezaji kunairudisha spirit ya timu enzi za ferguson, hii ni kutokana na sababu zifuatazo: 1. Wengi ya wachezaji wa Utd ni wadogo na waliamua kuichezea utd kwa kuamini falsafa za fagi kua yeye ndie mwenye uwezo wa kuipa mafanikio timu na kwa miongo 2 ya mafanikio ya utd kwa asilimia kubwa yamechangiwa na fagi, na kutokana na hivyo nivigumu kwa wachezaji hawa wachanga kuwabadilisha fikra zao kwa muda mfupi kuamini Moyes anaweza kuiendesha timu kwa mafanikio kama fagi kwa hiyo kuteuliwa kwa Giggs kinakua kiunganishi kikubwa kati ya Moyes na wachezaji na kwa asilimia kubwa imani na morali ya wachezaji na spirit yao itarudi kwa kuona ni jinsi gani Moyes anakubalika Utd sio tu kwa uongozi wa juu bali hata na wachezaji ambao wamewazidi kama Rio na Giggs wakiwa wao ndio roll model wao. 2. Kutokana na mabadiliko ya sasa ya michezo yote duniani kuwa kimaslahi au tuseme kibiashara zaidi, kwa timu kama Utd ambayo haipendezewi na mabadiliko haya ndani ya uwanja kutokana na utamaduni wao wa timu kwanza wachezaji na vinginevyo baadae hapa nazungumzia loyalty kwa wachezaji dhidi ya timu na loyalty ya kocha na utawala dhidi ya timu ni vigumu kupata wachezaji au makocha watakao kuwa na moyo wa kuipenda timu zaidi kuliko maslahi binafsi, kwa maana hiyo lazima utd itegemee makocha wazalendo kutoka kwa wachezaji wazalendo waliowatengeneza wenyewe na hapa ndipo unapata jibu la kwanini paul schools amebakishwa ktk bench la ufundi, kwa nini legends kama peter schmichel, edwin van der sar, eric cantona na wengineo wanakua ma ambersadors wa timu, pia unapata jibu la kwanini G. Nevill anatamka hadharani anataka kuwa kocha wa man utd kwa kipindi kirefu kama fagi, na unamalizia kwa kumuona Giggs anachaguliwa kuwa kocha mchezaji hii yote ni long term plan ya timu kutokana na utamaduni wa timu kulindwa ili utd iwe yenye mafanikio ya kujivunia siku zote. 3. Mwisho wa yote tunapata picha ya kuwa Giggs akiwa ndie mchezaji pekee ambae ameichezea utd kwa muda mrefu zaidi, kwa mafanikio zaidi na kwa moyo na mapenzi zaidi dhidi ya timu, haya ndio malipo ambayo utd inampatia sasa ukiwa mchezaji wa mpira popote duniani na ukilenga carrier yako ya soka wakati wa uchezaji wako mpaka kustaafu kwako iendelee kuwa hivyo hivyo basi man utd pekee ndipo utakapo timiza ndoto zako hii ni kwa wachezaji wa ndani ya utd na nje ya utd, kwani tumeshuhudia mara nyingi makocha mbali mbali ambao wamechezea timu na baadae kuja kuwa makocha katika timu hizo ndio ambao wameziletea mafanikio makubwa timu hizo kuliko makocha wote waliowatangulia mifano hai ni Pep Guardiola wa Barcelona na R. De Mateo wa chelsea ingawa wote hawakuthaminiwa na timu zao kwa kutowadhibiti na kuendelea kuwa nao. ® Hii inatupa picha kuwa kuteuliwa kwa Giggs kuna malengo makubwa nyuma ya pazia ambayo kwa kuangalia kwa jicho la tatu ndipo unaweza kuyaona na kugundua kuwa hii ni mipango endelevu ambayo utd imejiwekea na kuteuliwa kwake kwa kiasi kikubwa ile hofu ya wachezaji pamoja na mashabiki imeweza kuondolewa mara moja na wengi wetu tunaimani sasa Moyes anaweza kufanya kazi kwa amani kabisa na uongozi umelijua hili mapema na ndio maana uteuzi wake umeanza mara moja kabla timu haijajiandaa na maandalizi ya msimu mpya ili kuwe na mafahamiano mapema kwenye mazoezi pamoja na mechi za kirafiki kabla hatujaanza msimu.
Posted on: Fri, 05 Jul 2013 04:54:27 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015