Klabu ya Arsenal ilirejea kileleni mwa ligi kuu nchini Uingereza - TopicsExpress



          

Klabu ya Arsenal ilirejea kileleni mwa ligi kuu nchini Uingereza baada ya kulazimisha sare ya bao moja kwa moja na West Brom ambao waliwakosesha usingizi Manchester United juma moja lililopita.Wenyeji walikuwa wa kwanza kuliona lango la The gunners kwa Claudio Yacob kabla Jack Wilshere kusawazisha.Arsenal wana alama 16 sawa na Liverpool ambao wanadunishwa kwa wingi wa mabao.Tottenham nao waliaibishwa mbele ya mashabiki wao wa nyumbani baada ya kurindimwa mabao matatu kwa bila na West Ham.Kwingineko nguvu mpya Eden Hazard na Willian walitia kimyani bao moja kila mmoja na kuiwezesha Chelsea kuwanyuka Norwich mabao matatu kwa moja huku Southampon wakiwalaza Swansea mabao mawili bila jawabu. Chelsea ni watatu katika jedwali hilo la ligi na alama 14 sawa na Southampton,Mancity ni wa tano na alama 13,Spurs wa sita alama zikiwa 13 ila kwa uchache wa mabao wakifuatwa na Everton walio na 12,Hull city wanashikilia nambari nane alama zikiwa 11 kisha Manchester United ni wa tisa wakiwa na 10.
Posted on: Mon, 07 Oct 2013 03:30:29 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015