Kuna haja ya kuangalia upya mfumo wetu wa Elimu. Mwanzo sikutilia - TopicsExpress



          

Kuna haja ya kuangalia upya mfumo wetu wa Elimu. Mwanzo sikutilia maanani sana hiki kitu, kuna watu wanasema waliomaliza vyuo vikuu wasifikirie kuajiriwa badala yake wajiajiri. Kweli kujiajiri ni jambo zuri lakini kwa mfumo wa elimu yetu ni kazi sana(Siyo haiwezekani).Kwa msomi wa #Tanzania anaemaliza chuo kikuu na kujiajiri anahitaji mambo mengi sana kuyapata kama vile Inspiration na elimu ya ujasiliamali.Lakini kwa mazingira yetu ya kufundishwa na Prof. au Dr. ambae ameshindwa hata yeye kujiajiri/kuwa mjasiliamali then utarajie kutoa zao lenye uwezo wa kujiajiri au kuwa mjasiliamali binafsi bado napata shida kuamini hivyo(ingawa wapo walio weza). Mtaani ni tofauti kabisa na vyuoni ambapo wanafunzi tunawaza kazi nzuri na zenye mishahara mikubwa, kufungua makampuni na kuendelea kwa haraka haraka .Tunadanganyana na kupeana mifano ya baadhi ya watu waliofanikiwa Fast. Serikali na na baadhi ya watu wapendekeza wahitimu wakopeshwe mitaji na dhamana yao iwe ni VYETI(acha cheti chukua mkopo), wanafikiria kuwa tatizo ni mitaji lakini ninaamini mitaji bado siyo tatizo kubwa sana linalofanya wahitimu washindwe kujiajiri lakini mi nadhani tatizo ni mfumo na mentality zetu ndiyo tatizo kama mtu alishindwa ku-manage hela ya boom leo ukimpa 5M ataweza kweli. Mara ngapi wanafunzi wa kozi za uchumi na ujasiliamali wamshindwa ku-handle pesa zao. Kuna watu vyeti vyetu vitaozea kwenye Benki kwa sababu tuttapata mikopo lakini tutashindwa kuzalisha. Ila pia pamoja na hayo yote bado kuna jawabu moja kwa matatizo yetu nalo ni kumtegemea mungu na kuacha kuamini sana katika elimu za darasani badala yake elimu za madarasani ziwe ni chachu ya mapigano dhidi ya umasikini. Kwa karibu kabisa naona zama za Mhasibu kufanya kazi za uhasibu zinaanza kupotea na mhandisi kufundisha darasani zinajongea kwa haraka sana......
Posted on: Thu, 05 Sep 2013 21:09:21 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015