Kundi la Wanamgambo la Al Shabab latishia kufanya mashambulizi - TopicsExpress



          

Kundi la Wanamgambo la Al Shabab latishia kufanya mashambulizi Kenya iwapo itakaidi amri ya kuondoa Wanajeshi wao Somalia Kundi la Wanamgambo la Al Shabab lenye maskani yake nchini Somalia limetoa kitisho cha kufanya shambulizi jingine nchini Kenya kutokana na Serikali ya Nairobi kugoma kuondoa wanajeshi wake huko Mogadishu wanaopambana kulitokomeza kundi hilo. Al Shabab kupitia taarifa yao wamesema iwapo Serikali ya kenya itakaidi amri yao ya kuwataka waondoe wanajeshi wao basi wenyewe wataendelea kuandaa na kutekeleza mashambulizi zaidi katika Jiji la Nairobi hadi pale watakaposikilizwa. SOMA ZAIDI mussashimba.blogspot/2013/10/kundi-la-wanamgambo-la-al-shabab.html#links
Posted on: Wed, 02 Oct 2013 17:04:50 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015