Kutoka ndoto ya Msoga hadi ndoto ya Tanzania na Afrika katika - TopicsExpress



          

Kutoka ndoto ya Msoga hadi ndoto ya Tanzania na Afrika katika medani za kimataifa. Jakaya Mrisho Kikwete,mtu wa kawaida,mpenda watu,mkarimu,mcheshi,mwenye maono na subira iso kifani,utumishi wako uliotukuka kwa taifa letu la Tanzania umetupa heshima kubwa Afrika na duniani.Umefanya mambo makubwa katika uongozi wa awamu yako pengine kuliko yaliyofanywa tangu uhuru wa nchi hii upatikane Desemba 9,1961. Tulikuwa na barabara za lami KM 6000 tangu uhuru hadi mwaka 2005 wakati unaingia madarakani,lakini katika utawala wako pekee umejenga zaidi ya KM 11,000 za lami,tulikuwa na wanafunzi wa vyuo vikuu 40,000 tangu Uhuru hadi mwaka 2005 wakati unaingia madarakani,lakini katika kipindi chako pekee idadi imekuwa 120,000(mara 3 zaidi). Umekuwa mwana demokrasia wa hali ya juu uliyelipatia jawabu tatizo la mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar ambapo kwa mara ya kwanza tangu mfumo wa vyama vingi,uchaguzi umefanyika Zanzibar bila ya fujo wala damu na serikali ya umoja wa kitaifa imeundwa(si jambo jepesi).Maalim Seif Shariff Hamad na Prof Lipumba atakubaliana nami katika jambo hili. Ni Rais pekee tangu uhuru, uliyetoa uhuru mkubwa wa habari na vyama vya siasa kufanya kazi zao,hadi kufikia hatua ya wanasiasa na wanahabari kuvimbiwa na uhuru huo. Umekuwa kiongozi msikivu na mwenye maono,ambae umeamua watanzania tuanze mchakato wa kupata katiba mpya ya nchi yetu,jambo ambalo limewakuna wadau wengi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wanazi wa katiba mpya,huku wengine wakidhani katiba iliyopo ndio kikwazo pekee cha wao kuingia ikulu,hao hawakukuumiza kichwa kamwe.Uliwaalika,ukapokea maoni yao na ukanywa nao chai bila kujali jana yake walisema hawakutambui kama Raisi wa nchi hii.Nadhani kwa hili Dr. Slaa,katibu mkuu wa Chadema atakubaliana nami. Umekuwa mwanadiplomasia mahiri na mfuasi mkubwa wa umajumui wa Afrika ambaye katika kipindi chako pekee, Tanzania imepaa juuu katika duru za kimataifa na heshima ya Dunia,kiasi cha kufikiwa na viongozi watatu wa dola kubwa duniani katika awamu ya nne pekee.Rais Bush,XI JINPING na Obama.Wenye tabia ya ukasuku wanaweza kuona hili ni jambo la mzaha,lakini kwa wenye kufikiri kwa kina na wasomi,tunajua manufaa ya safari hizi kwa taifa.Nina imani hata bwana Freeman Mbowe atakubaliana nami kwenye hili. Umekuwa kiongozi mpigania amani na ustawi wa Afrika,ambapo katika utawala wako pekee tumeshuhudia jeshi letu likifanya utumishi mahiri na wenye kutukuka katika harakati za kutunza amani Darfur-Sudani,ukombozi wa visiwa vya Anjuani-Comoro,amani Lebanon na sasa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mara zote umekuwa mtu wa watu na Uraisi wako haujakutenganisha na watu wa kawaida wala kukufanya usahau ulikotoka.Watanzania kote unakopita na sisi wengine tuliopata kuwa karibu yako kwenye shughuli na hafla mbalimbali au familia yako tunajua jambo hili.Wakati mwingine walinzi wako wamekuwa wakipata wakati mgumu kutokana na hulka yako na mapenzi yako kwa watu wako.Umekuwa ukipokea simu na kujimu ujumbe mfupi wa simu kutoka kwa watanzania wa kawaida kabisa wanaokupigia na kukutumia ujumbe,wakati mwingine hata ikiwa usiku mzito.Jambo hili watu wengi hawaliwezi,wakiwemo wasaidizi na watu wako wa karibu. Jakaya Khalfani Mrisho Kikwete,Raisi wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,ukiwa kijana msomi kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam,ulijitolea kwenda kukitumikia chama chako cha TANU katika wakati ambao nchi ilikua na wasomi wachache na nafasi za ajira kubwakubwa zenye malipo makubwa zilikua nyingi mno.Uliishinda tamaa na ukaweka mbele uzalendo na mapenzi kwa chama chako,jambo ambalo wengi hawakuliweza. Wewe ni mwanasiasa mashuhuri,kiongozi,mwanadiplomasia na mwanademokrasia wa kweli wa Tanzania na Afrika.Unastahili kukumbukwa na vitabu vya historia,unastahili kupata tuzo yoyote iwayo kwa utumishi wako uliotukuka. Mungu ibariki Afrika,Mungu ibariki Tanzania.
Posted on: Fri, 26 Jul 2013 13:17:53 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015