Kutokana na hati ya mashtaka iliyotolewa na Idara ya Pili ya - TopicsExpress



          

Kutokana na hati ya mashtaka iliyotolewa na Idara ya Pili ya Uendeshaji Mashtaka, Liu alitumia nafasi yake na kuwasaidia watu 11 kupata vyeo na mikataba ya ujenzi. Pia waziri huyo alipokea rushwa ya dola za kimarekani milioni 10.53 kutoka kwa watu hao kati ya mwaka 1986 hadi 2011. Akiwa waziri wa reli, Liu anatuhumiwa kumsaidia Ding Yuxin na ndugu zake kushinda zabuni za usafirishaji wa mizigo na ujenzi wa njia za reli, pia anashukiwa kuwasaidia kupata hisa katika kampuni ya treni za mwendo kasi na kufadhili viwanda. Liu alifanya hivyo kwa kuvunja kanuni na kutoa upendeleo, ambavyo viliwaruhusu Ding na familia yake kupata faida kubwa. Hati hiyo ya mashtaka inasema matumizi mabaya ya madaraka yaliyofanywa na Liu yalisababisha uharibifu mkubwa wa mali za umma na athari mbaya kwa taifa la China na wananchi wake. Hati hiyo inataka Liu afunguliwe kesi ya uhalifu wa kupokea rushwa na matumizi mabaya ya fedha. Liu aliondolewa madarakani mwezi Februari mwaka 2011 kwa tuhuma za ukosefu wa nidhamu, na mwaka jana alifutiwa uanachama wa Chama cha Kikomunisti cha China. Inaaminika kuwa, huenda Liu aliondolewa madarakani kutokana na ajali mbaya ya treni iliyotokea mwezi Julai mwaka 2011 na kusababisha vifo vya watu 40 na kujeruhi wengine 172. Karibu watu 50 walifika mahakamani kusikiliza kesi hiyo wakiwemo familia ya Ding, waandishi wa habari, wabunge, na washauri wa masuala ya kisiasa. Hukumu ya kesi hiyo ndio iliyomfanya anyongwe. source BBC
Posted on: Fri, 12 Jul 2013 14:30:47 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015