LUSAKA Waziri wa Ulinzi nchini Zambia ametangaza kuwa, watu 45 - TopicsExpress



          

LUSAKA Waziri wa Ulinzi nchini Zambia ametangaza kuwa, watu 45 wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kushiriki katika harakati za kudai kujitenga mkoa wa Barotseland magharibi mwa nchi hiyo. Geoffrey Mwamba ameyasema hayo na kuongeza kuwa, watu hao wanaendelea kushikiliwa na polisi ya nchi hiyo, kwa tuhuma hizo na kwamba, Watuhumiwa hao watapandishwa kizimbani hii leo ili kusomewa mashitaka dhidi yao Ameongeza kuwa, watu hao 45 ni miongoni mwa wanaharakati wa Barotseland na kwamba, walitiwa mbaroni katika mkoa huo. Serikali ya Lusaka inawatuhumu watu hao kwa kufanya za kuzusha machafuko na kutundika bendera ya Barotseland magharibi mwa nchi hiyo. Mwaka jana Rais Michael Sata wa Zambia, alilitaka jeshi kukabiliana na mtu yeyote atakayetaka kuanzisha nchi nyingine kwa jina la Barotseland.
Posted on: Tue, 20 Aug 2013 05:11:53 +0000

Trending Topics



5

Recently Viewed Topics




© 2015