MAKALA YANGU YA DARFUR (SEASON 2) Baada ya kusafiri kuelekea - TopicsExpress



          

MAKALA YANGU YA DARFUR (SEASON 2) Baada ya kusafiri kuelekea nchini Sudan katika jiji la DARFUR, sasa nimerudi Tanzania. Nimefungua mtandao wa kijamii wa facebook na kukutana na mtu ambaye ni tapeli, mtu ambaye alinitumia meseji na kusema kwamba yeye alikuwa ni msichana ambaye amefiwa na baba yake na yupo kwenye kambi ya wakimbizi nchini Senegal. Kanitumia picha nyingi nzuri baada ya kumpa email yangu. Alisema nimpe akaunti yangu ili anitumie pesa, nikampa akaunti iliyokuwa na shilingi laki tano kwa ajili ya kuona kipi kingetokea. Kilichotokea, fedha zangu zikaibiwa. Nilifanya vile makusudi. Baada ya kufanya kazi ya uandishi wa habari na BBC, kitengo cha kijasusi cha CIA cha nchini Uingereza kimeniajili kwa ajili ya kufanya kazi ya kijasusi nchini Iraq, ila kabla ya kuanza kazi, wamenituma nimtafute mtu yeyote ambaye ni tapeli wa mitandaoni, yote hiyo ni kuona kama nimeiva. Sasa huyu kajiingiza, kajitambulisha kwa jina la ANNASTAZIA MICHAEL. Huyu ndiye nitaanza nae, huyu ndiye atakayenifanya nisafiri kuelekea huko Senegal japokuwa nilikuwa na uhakika kwamba yeye ni Mnigeria. Nitaanza kwenda huko Senegal na kisha kuelekea nchini Nigeria kumtafuta. Kama ni mafunzo makubwa ya kompyuta, nimekwishapewa. Sasa ndio kazi inaanza, nikifanikiwa, nitaelekea nchini Iraq kwa ajili ya kuchunguza uwepo wa mabomu ya nyuklia. Hii ni Tamthilia ambayo inaendelea facebook. Season ya kwanza ilikuwa ni kwenda kule Darfur, sasa inaingia season ya pili ambayo nitaanza kumtafuta tapeli wa mtandaoni. Ikiisha, itaanza ya tatu na kuendelea. Hii ni tamthilia yenye season sita mpaka ikamilike. Kama uliwahi kuisoma MAKALA YANGU KUTOKA DARFUR....hii utaifurahia zaidi. MAKALA KUTOKA DARFUR (SEASON YA PILI). WANGAPI WAPO TAYARI KUISOMA MAHALI HAPA?
Posted on: Fri, 16 Aug 2013 15:15:05 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015