MATUKIO ya utekaji, kupiga na hata kuuawa kwa viongozi na - TopicsExpress



          

MATUKIO ya utekaji, kupiga na hata kuuawa kwa viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani, hususan CHADEMA, yamechukua sura mpya baada ya shirika moja la Kijerumani kutoa ripoti iliyoanika hadharani ukatili huo. Ripoti hiyo ambayo inadaiwa kusambazwa ndani na nje ya nchi, imeshutumu vikali matukio hiyo, huku ikisukuma lawama kwa vyombo vya dola kwa kushindwa kuchukua hatua madhubuti dhidi ya watu wanaodaiwa kuhusika na ukatili huo. Shirika la Konrad Adenauer Stiftung la Ujerumani linalojihusisha na utafiti wa siasa nchini limetoa ripoti hiyo, huku likitahadharish a kuwepo kwa uwezekano mkubwa zaidi wa vitendo vya kikatili kwa viongozi wa vyama vya upinzani, wanaharakati na wakosoaji wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete kadiri chaguzi zinavyokaribia. Ripoti hiyo iliyoandikwa na Danja Bergman na Stefan Reith, iliyotolewa tangu mwezi uliopita, inazungumzia matukio mbalimbali yaliyolikumba taifa la Tanzania kwa siku za karibuni, huku suala la bomu la Arusha lililolipuliwa katika mkutano wa CHADEMA likionekana kulitia doa taifa la Tanzania katika medani za kimataifa. Hata hivyo, wachunguzi hao wana maoni kuwa ongezeko la matumizi ya mabavu kutoka kwa vyombo vya dola dhidi ya maandamano halali na ukosoaji, ni dalili tu ya mambo makubwa zaidi yanayoweza kutokea katika kipindi cha miaka miwili ijayo, wakati uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika. Ripoti hiyo pia inasema, kwa kadiri ya hali ilivyo kila aina ya vitisho, udanganyifu na matumizi ya mabavu vitakuwa vikibadilishwa badilishwa na kutokea katika sura tofauti ikiwemo vurugu ili kupotosha umma, huku watuhumiwa wa vurugu hizo wakishindwa kutambuliwa, na wale wanaotambuliwa watafichwa au kutochukuliwa hatua zozote za kisheria na mamlaka husika. Limeenda mbali zaidi na kusema kuwa hata pale vyombo vya dola vinapohusishwa na mauaji, kwa ushahidi wa wazi, watuhumiwa wamekuwa wakilindwa na kuendelea kutesa mitaani bila kuchukuliwa hatua zozote za kisheria, badala yake wahanga wa matukio hayo wamekuwa wakishitakiwa kwa kesi mbalimbali za kubambikiza, zikiwemo za uchochezi, ugaidi, na kuhamasisha chuki kati ya wananchi na serikali yao. Katika uchaguzi mdogo uliofanyika nchini Juni 16 katika kata 22 na Julai 14 katika kata nne za Arusha, vurugu nyingi ziliripotiwa zikiwahusu wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuteka, kujeruhi na kupewa mafunzo ya kijeshi kwa ajili ya kusimamia shughuli za ulinzi katika chama hicho kikongwe nchini. Wachunguzi wa masuala ya siasa wanaona matokeo ya uchaguzi uliofanyika hivi karibuni yanaonyesha kuwa Chama kikuu cha upinzani nchini (CHADEMA) kinapata ustawi wa kasi kubwa, hivyo kuwa tishio katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014 na Uchaguzi Mkuu wa 2015, jambo ambalo linakiogopesha chama kinachotawala. Ripoti hiyo inasema upinzani umefanikiwa kujiweka kama serikali mbadala inayoonekana katika chaguzi tangu 2010, hivyo kuna wasiwasi kuwa watawala watatumia kila walichonacho mikononi mwao kuzuia mabadiliko hayo yasitokee.
Posted on: Wed, 17 Jul 2013 16:00:57 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015