MFUNZO KWA WANADIJITALI: Subow,mwanashati,mfuauji na mlimbwende - TopicsExpress



          

MFUNZO KWA WANADIJITALI: Subow,mwanashati,mfuauji na mlimbwende sana,aliona Subay,mke nadhifu,mrembo na maridadi zaidi.Ndoa yao ilikuwa murua na arusi yao ilinawiri na kushamiri sana.Kwa jumla tamasha ilifana.Waliishi.Baada ya siku kadhaa ndoa yao ikaingia doa.Wakawa hawasemezani wala hawaongeleshani.Cheko na bashasha zao zikayeyuka kama mawingu ya jangwani. Subow akitoka kazini,kimya cha kaburi.Subay naye kanuna kando-watani husema kauma jongoo.Au kanuna kama shetani. Siku moja Subow alitoka matembezeni.Alichoka sana.Saa nane baada ya kishuka aliamua ajipumzishe kidogo kitandani akisubiri saa kumi na mbili aingie kazini shifti au zamu ya usiku.Alijua usingizi ungemwiba na huenda akalala fofofo achelewe kuenda kazini.Lakini afanyeje ilhali yeye na mkewe hawasemezani.Potelea mbali!Liwalo na Liwe!. Akatwaa kipande cha karatasi akaandika:"MKE WANGU,ZIKIFIKA SAA KUMI NA MOJA UNUSU UNIAMSHE NIENDE KAZINI".Kikaratasi hicho chenye arafa,akakitupa wazi bila kukikunja juu ya meza.Akaenda kitandani na kujibwaga. Subay alipokwenda ukumbini,akakisoma.Mnh!Naam,ilipotimu saa kumu na moja unusu,mkewe mtu naye akatwaa kipande cha karatasi na kuandika,"MUME WANGU,SAA KUMI NA MOJA UNUSU ZIMETIMIA,AMKA UENDE KAZINI", Yule Subow aliupata usingizi wa pono.Akalala fofofof mpaka saa moja jioni.Kachelewa kazini tayari.Alipoamka,nikwambie nini?Sijui tu.Labda wewe uniambie. JE NI KOSA LA NANI? KUMBUKA HII NI SHIDA YA MAPENZI YA DIJITALI.
Posted on: Wed, 18 Sep 2013 09:35:09 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015