MGOGORO WA RWANDA NA TANZANIA NI BAINA YA VIONGOZI. KATIBU Mkuu - TopicsExpress



          

MGOGORO WA RWANDA NA TANZANIA NI BAINA YA VIONGOZI. KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk Willibrod Slaa amesema anaamini Rwanda haitathubutu kuigusa Tanzania kwa kuwa ni nchi yenye amani na upendo. Dk Slaa aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam katika kongamano la Uchumi na Ajira kwa Vijana, ambapo alisema mgogoro huo kati ya Rwanda na Tanzania haoni kama ni wa baina ya nchi na nchi bali ni wa viongozi wenyewe, hivyo ni jambo la busara kuyamaliza wenyewe. “Nchi zisiingizwe katika migogoro bali wakae wenyewe viongozi kama wana matatizo yao wayamalize bila kuziingiza nchi, si busara matatizo ya watu wawili yaziingize nchi katika migogoro, “alisema Dk Slaa. Kauli hiyo ya Dk Slaa imekuja siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kueleza kuwa Tanzania haina mgogoro na nchi ya Rwanda, kutokana na kauli za kejeli na matusi zilizokuwa zikitolewa na viongozi wa nchi hiyo dhidi yake na Tanzania. Katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi ya kuzungumza na Taifa, Rais Kikwete alisema yeye binafsi na Serikali kwa ujumla haina ugomvi wala nia yoyote mbaya na Rwanda. “Nawahakikishia ndugu zangu wa Rwanda kuwa kwa upande wetu hakuna kilichobadilika wala kupungua katika uhusiano wetu. Mambo yapo vile vile. Kwa upande wangu binafsi sijasema lolote kuhusu Rwanda pamoja na maneno mengi ya matusi na kejeli yanayotoka kwenye vinywa vya viongozi wa Rwanda dhidi yangu,” alisema Rais Kikwete katika hotuba yake.
Posted on: Sun, 04 Aug 2013 08:00:18 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015