MTOTO AOZWA TOA MAONI JINA NA MAHALI Ofisi ya Mkuu wa Wilaya - TopicsExpress



          

MTOTO AOZWA TOA MAONI JINA NA MAHALI Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma inatarajia kumfikisha Mahakamani Bwa Mtemi Mhundi anayedaiwa kumuozesha Mtoto wake mwenye umri wa miaka 11 baada ya kupewa mbuzi 11 Akiongea na waandishi wa habari ofsini kwake Mkuu wa Wilaya hiyo Bi Betty Mkwasa amesema kuwa baba wa mtoto huyo alimuozeshwa kwa bwanaOmar Mwani ambaye ni mtoto wa dada yake , ili mali hiyo isiende nje ya ukoo Bi Mkwasa amesema kuwa Mtoto huyo ambaye jina lake tunalihidhi ,alishindwa kuhimili ndoa hiyo kutokana na umri wake na hivyo aliamua kutoroka kwa bwana huyo na kukimbilia kwa Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Mkonde kikichopo wilayani humo. Star tv ikalazimika kuongea na Bwana Mtemi Mhindi ambaye ndiye aliemuozesha mtoto huyo,na kumnyima haki yake ya msingi ya kwenda shule, bila wasiwasi anakili kutenda kosa hiyo Elia Ndahali ni baba mdogo wa mtoto huyo yeye anasema wakati kaka yake anamuozesha mtoto huyo alimficha Mtoto huyo ambaye hivi sasa anaishi na Mkuu wa wilaya ya Bahi,anaonekana kutokuwana imani na watu wote hasa wanaofika nyumbani kwa kiongozi huyo na hata tulipohitaji kuzungumza naye alikataa Ndipo inanibidi nimtafute wakili wakujitegemea na Mwendesha Mashitaka waSerikali Mkoani Dodoma Bwana Emmanuel Meta ili basi alezee iwapo baba mzazi atapatikana na hatia adhabu yake itakuwaje Hiyo ni adhabu kwa Baba Mzazi lakini kwa upande wa mwanaume aliekuwa akiishi naye ambaye amekimbia mpaka sasa na ajulikani alipo, iwapo atapatikana na kufikishwa katika vyombo vya sheria adhabu yake nikifungo cha miaka thelathini ,na kitendo hicho kinantafasiriwa kama Ubakaji. MWISHO
Posted on: Tue, 08 Oct 2013 16:30:30 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015