MTU KABLA HAJAOKOKA ANAONEKANA KATIKA MITAZAMO MIWILI - TopicsExpress



          

MTU KABLA HAJAOKOKA ANAONEKANA KATIKA MITAZAMO MIWILI ISIYOFAA: 1.kama mfu yaani amekufa WAEFESO 2:1-3[Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu, ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kumfuata mfalme wa uwezo wa anga , roho yule ataendaye kazi sasa katika wana wa kuasi, ambao zamani sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapendi ya mwili na ya nia tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine} 2.MPOTEVU yaani ulikuwa umepotea LUKA 15:4{Ni nani kwenu mwenye kondoo mia akipotewa na mmoja wapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hata amwone?} Hivyo mtu mwenye dhambi anafananishwa na: 1.kondoo aliyepotea LK:15:4-7 2.shilingi iliyopotea LK 15:8-10 MUNGU akubariki sana na MUNGU akupe nguvu na ujasiri ili umpe YESU maisha yako maana hakuna uzima kwingine popote nje na YESU KRISTO.(Yohana 14:6, Matendo 4:12) Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula.
Posted on: Thu, 15 Aug 2013 05:56:05 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015