Manongi alisema kampuni za ndege zimeagizwa kufanya mabadiliko ya - TopicsExpress



          

Manongi alisema kampuni za ndege zimeagizwa kufanya mabadiliko ya ratiba za safari siku atakapowasili Rais Obama ili kutoa nafasi kwa anga hilo kutumika kwa shughuli za mapokezi yake. Alisema kampuni zote za ndege zimeshapewa taarifa kuhusu hatua hiyo. “Kubadilishwa kwa ratiba kunatokea mara kwa mara na huwa tunawapa taarifa kampuni za ndege mapema ili wajue namna ya kujipanga,” alisema Manongi. Kutua Senegal leo Rais Obama anatarajiwa kuanza ziara yake ya barani Afrika leo na alitarajiwa kutua Dakar, Senegal saa 9.30 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki.
Posted on: Wed, 26 Jun 2013 07:04:27 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015