Mfumo wa uongozi katika taifa hili unafaa kufanyiwa marekebisho - TopicsExpress



          

Mfumo wa uongozi katika taifa hili unafaa kufanyiwa marekebisho ili kuepuka hulka ya jamii yenye watu wengi kuongoza kila wakati kunapofanyika kwa uchaguzi mkuu.Iwapo mfumo huu wa uongozi utabatilishwa,kila jamii kote nchini itapata fursa ya kuongoza taifa hili kwani kutakuwa na nafasi sawa.Muungano wa CORD sasa uko mbioni kutafuta uungwaji mkono kuwezesha kufanyika kwa kura ya maoni ili kutoa fursa kufanyika kwa uchaguzi utakaopelekea kurekebishwa kwa katiba.Iwapo hili litafaulu,haya yatakuwa marekebisho ya kwanza kufanyiwa katiba tangu kuidhinishwa kwake mwaka 2010.Mfumo huu wa uongozi unaelekeza kuwa kiongozi wa chama au mrengo wenye wengi bungeni ndiye anafaa kuwa rais wa taifa kama inavyofanyika katika mataifa ya India,Ukrain,Japan na Italia.Kwa mujibu wa sheria,ili sheria kurekebishwa,ni lazima wakenya watoe uamuzi kwa kushiriki katika kura ya maoni.
Posted on: Mon, 12 Aug 2013 06:20:36 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015