Mheshimiwa Mwenyekiti Wa Mabadiliko ya Katiba, K.n.y. Wapiganaji - TopicsExpress



          

Mheshimiwa Mwenyekiti Wa Mabadiliko ya Katiba, K.n.y. Wapiganaji wa Mapambano ya kudumusha fikra sahihi za Baba wa Taifa, kwa heshima na taadhima, na kwa unyenyekevu mkubwa, naomba kuwasilisha Maoni na Mapendekezo ya Wapiganaji kwa Tumeyako Tukufu ya mabadiliko ya Katiba ambayo ni muhimu kama dira mwelekeo na Mwongozo wa Taifa letu kwa maslahi ya Watanzania wa hivi sasa na vizazi vijavyo. Tunatanguliza shukrani kama maoni yetu yaatapewa nafasi bila kupuuzwa. Tunaamini kuwa: Tume yako ya Mabadiliko ya Katiba itawezesha Wananchi kupata katiba ambayo Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii ambayo itaunda Serikali yao wenyewe kwa ajili ya masilahi yao kwa haki na uhuru kabisa itakayoongoza Taifa letu kwa kuzingatia misingi ya ujamaa, ambayo ni pamoja na demokrasia ya kweli, uwazi, kupiga vita ukoloni Mamboleo, kupiga vita uharibifu, ubadhilifu na wizi wa uma, na itakayozingatia uwakibikaji kwa mujibu wa misingi ya uongozi bora, ambao ni pamoja uongozi wa sheria, haki za Wananchi, haki za binadamu, isiyokuwa na dini na isiyokuwa na ama upendeleo au ubaguzi wa aina yo yote ile. Mungu atusaidie. Watanzania wanataraji kuunda Katiba madhubuti ya Mapinduzi yenye uwezo mkubwa, wa kuongoza mapambano ya Wananchi katika mazingira mapya ya wakati huu na ya wakati ujao na hasa ya kutoka kwenye unyonge wa kunyonywa, kunyanyaswa, kupuuzwa na kudharauliwa na kufikishwa katika hali ya nguvu, ya uhuru wa kweli na kuheshimiwa ili tusionewe tena, tusinyonywe tena tusipuuzwe tena na wala tusidharauliwe tena. Watanzania tumeamua kuunda Katiba iliyo madhubuti yenye misingi na uwezo mkubwa wa kuongoza mapambano yao ya vita vya kulitoa Taifa letu katika hali ya unyonge na kulitia katika hali ya nguvu. Vita vya kufanya Wananchi wa Tanzania watoke katika hali ya dhiki na kuwa katika hali ya neema. Watanzania wanataji kuunda Katiba madhubuti ya Mapinduzi, yenye uwezo mkubwa wa kuongoza mapambano ya kudumu dhidi ya Ukoloni Mamboleo, ubepari na unyonyaji, dhidi ya wapinga maendeleo na wababaishaji wa kisiasa, dhidi ya wahujumu uchumi, majambazi, wezi, wazururaji, wazembe, dhidi ya waharibifu na wabadhirifu wa mali za umma, Watanzania wanataraji kuunda Katiba madhubuti ya Mapinduzi, yenye uwezo mkubwa ya kuaandaa mipango maalum ya kuwafundisha Viongozi Serikalini tangu ngazi ya Taifa hadi ngazi wa mitaa na viongozi katika Vyama vya siasa, vyama vya Wafanyakazi, Asasi zisizokuwa za kiserikali ili waelewe siasa yetu na mipango ya uchumi. Msingi wa Katiba hii unasisitiza weledi na kuwa Viongozi lazima wawe mfano mzuri kwa Wananchi kwa maisha yao na vitendo vyao pia. Watanzania wanataraji kuunda Katiba madhubuti ya Mapinduzi yenye uwezo wa kutuwezesha Watanzania na hasa viongozi kujiamini kifikra, katika mapambano dhidi ya mbinu za maadui wetu, hasa Mawakala wa Wakoloni Mamboleo, vibepari na vibwenyenye wanazozitumia katika vita vya ghiliba dhidi ya Ujamaa na kututaka tubadilishe mwelekeo wetu wa uchumi tufuate sera potofu za ubepari wakati huo huo wao wakijua kwamba wayasemayo si kweli. Watanzania tunaunda Katiba yenye Msingi wa uhuru kamili wa kujitegemea ambao ni pamoja na kujiamini kifikra kwa msimamo kwamba kitendo cha sisi Watanzania kufanya maamuzi yetu sisi wenyewe ni kitendo cha Maendeleo japokuwa hakituondolei njaa na wala hakituletei shibe. Ifahamike kuwa kwa mujibu wa masharti ya msimamo huu, Watanzania tunawajibika kuzingatia uchumi wa nadharia ya Ujamaa na kujitegemea, na wala tusirudi nyuma, ama sivyo tukirudi nyuma tutageuka kuwa jiwe. Msimamo sahihi wa mapambano unaotokana na nadharia sahihi ya Ujamaa utawezesha uchumi wetu kuimarika na baadhi ya matatizo yetu ya uchumi yatatatuliwa na kutuepusha maamuzi na vitendo ambavyo vinarahisisha ama kuoteshwa kwa mizizi ya ubepari au kuwezesha Wakoloni Mamboleo kututawala kiuchumi japokuwa watatuachia uhuru wa bendera tu. Watanzania wanataraji kuunda Katiba madhubuti ya Mapinduzi yenye uwezo mkubwa wa kujenga utamaduni wa kutanguliza utaifa kwanza na kutumia nguvu za Serikali, Vyama vya Siasa na vyama vya wafanyakazi kuweka pumzi ya kujenga uzalendo, kupenda kufanya kazi, kuthamini kazi, uaminifu na kupiga vita uharibifu na ubadhirifu wa mali za umma pasipo kutanguliza masilahi binafsi kwa maksudi kabisa ili kuwawezesha Wafanyakazi kuwa na utamaduni wa kushiriki kwa dhati katika harakati zao, ili waongeze juhudi yao kazini wakitambua kuwa sehemu zao za kazi ndiyo uwanja wao wa kuinua hali yao ya maisha na mapambano ya kujenga Ujamaa, Watanzania twanataraji kuunda Katiba iliyo madhubuti na vile vile kutambua kwamba tunaweza kujenga uchumi imara, tunaweza kumiliki viwanda, na tunaweza kupata fedha, lakini msingi wake ni WANANCHI na JUHUDI zao na sio fedha za wageni kutoka ng’ambo. Tanzania itajengwa na Watanzania wenyewe, wenye moyo na hasa walio wazalendo. Ifahamike kuwa Watanzania wanataraji kuunda Katiba madhubuti ya Mapinduzi yenye uwezo mkubwa wa kujenga utamaduni wa kuwawezesha Wananchi na hasa Viongozi, kuwa makini katika kuchagua silaha ya mapinduzi tunayoyataka. Katiba hii inatuwezesha kufahamu kuwa ni fikra potofu kuamini kuwa tunaweza kuondoa unyonge wetu kwa kutumia silaha ya wenye nguvu, silaha ambayo hatuna. Ni dhahiri kwamba ni makosa kuchagua fedha kama silaha yetu. Fedha ni mojawapo ya matunda ya maendeleo lakini sio Msingi wa Maendeleo. Watanzania Wanataraji kuwa Katiba iliyo madhubuti katika misingi ya kufutilia mbali matabaka kulingana na hali ya maisha na aina zote za unyonyaji nchini na kuziba mianya ya jaribio lolote lile la mtu kumuonea mtu au shirika au chombo cha nchi kuonea na kudhalilisha mwananchi, kudhoofisha uchumi na kuzorotesha maendeleo ya Taifa. Hii ni Katiba iliyo wazi kwamba ubepari ni unyama na tutaendelea kupiga vita ukoloni mamboleo na jaribio lolote la kuwagawa Watanzania kwa misingi ya kidini, ukabila, rangi na ubaguzi wa aina yoyote ile. Watanzania Wanataraji kuwa Serikali ya Watanzania itaundwa na Watanzania wenyewe kwa ajili yao wenyewe. Wananchi wataunda Serikali yao ambayo itawajibika kuimarisha uchumi na heshima ya Taifa lao, na Serikali itakayozingatia uongozi bora, ambao ni pamoja na kuzingatia misingi ya demokrasia ya kweli, uwazi, uongozi wa sheria, haki za Wananchi na kudumisha viwango vya haki za wananchi na kwa kadri ya viwango vya haki za binadamu vinavyokubalika kimataifa. (The state shall undertake to abide by the principles of good governance, including adherence to the principles of democracy, transparency, the rule of law, social justice and the maintenance of universally accepted standards of human rights) Wapiganaji wanaamini kuwa Tanzania itajengwa na Watanzania wenyewe wenye moyo na hasa walio wazalendo. Kwa madhumuni ya tafsiri halisi ya Katiba hii, wanapendekeza kuwa endapo patakuwa na utata katika tafsiri ya ibara yoyote ile, tafsiri kutokana na Katiba iliyoandikwa katika lugha ya Taifa (Kiswahili) itahesabika kuwa tafsiri sahihi. Zidumu Fikra Sahihi za Baba wa Taifa Leo siku ya 30 ya Mwezi wa nane Mwaka 2013 …………………………………………………….. K.n.y. Wapiganaji ………….. Dr. Kalokola Muzzammil Mwenyekiti wa Wapiganaji wa Mapambano ya kudumisha Fikra Sahihi za Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere Idealogy Conservation Society. Cell:- 0784 489 526, 0713 330 633; 0774 399 526 e-mail:- zidumufikrasahihizababawataifa@yahoo
Posted on: Tue, 03 Sep 2013 15:00:58 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015