Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo ameutangazia umma wa - TopicsExpress



          

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo ameutangazia umma wa watanzania kuwa "Watuhumiwa walioingiza mabomu ya kurushwa kwa mkono yaliyorushwa Arusha Kanisani na kwenye Mkutano wa Chadema Soweto mwezi Mei na Juni mwaka huu wamekamatwa" Sijui msemaji wa Polisi Arusha ni nani hasa... ingawa Magesa (Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi) amedai RPC atataja majina hayo hivi karibuni, which means Polisi hawajatoa taarifa yoyote bado. Tafsiri ya haraka hapa ni kwamba, wahusika wa milipuko yote miwili ni wamoja. Hii inanireesha kwenye speculation zangu za awali kuwa kwa jinsi hali ilivyokuwa..ilikuwa ni rahisi sana kuamini mlipuko wa kanisani ulikuwa ni maandalizi tu ya kuwaweka watu wa Arusha na watanzania wengine wazoee hali ya milipuko ili yakitokea kwa Chadema isiwe ajabu sana.. hili bado naendelea kuamini liko hivyo! Utakumbuka mapema baada ya mlipuko kwenye mkutano wa Chadema, kuna timu za uchunguzi zilitoa taarifa kuwa mabomu yake yametoka China na sio ya kienyeji. Angalau sasa RC amedai wamekamata "watuhumiwa walioyaingiza" labda angemalizia tu "kutoka China" Uongo ukatungwa na kupambwa kuwa kuna FBI walikuja nchini kuchunguza milipuko hiyo.. Wakakamatwa waAsia wako na safari zao tukaambiwa ni washukiwa na mwishowe mwendesha bodaboda chalii mdogo akabebeshwa kesi zote 21 kuwa ndie muhusika wa mlipuko wa Olasiti... Juzi Kati tuliona Balozi wa China nchini akifanya kazi ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM.. Huyu kwasababu wako nae meza moja kama walivyoshirikiana nae kuwahadaa wananchi kinyume na misingi ya kidiplomasia, basi wamshirikishe asaidie kuvujisha siri ni kontena lipi liliruhusiwa huko kwao na lilielekezwa kwa nani.. Kama ilikuwa ni shehena ya silaha za Jeshi au Polisi aseme pia ili iwe rahisi kumtafura kama ni askari alinyofoa huto tubomu tuwili na kuja kuua watanzania. Swali gumu kujibu ni kina nani wanamiliki mabomu nchini kiasi cha kuwa na chuki ya kuuwa watu wa Chadema na waumini wa kikristo?? Ukweli Daima Utadhihiri.. Ni Swala la Muda Tu! Mungu aziweke roho za marehemu wote mahala pema, na awajalie ujasiri wa kusonga mbele majeruhi wote na wale waliopoteza wapendwa wao. Shetani awapokee na asiwaachie wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine kufanikisha ukatili huu wa makusudi kabisa na laana ya Mungu iwe juu yao!!
Posted on: Wed, 18 Sep 2013 11:04:57 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015