Moja kati ya vyanzo vya mapato vya klabu ni makumbusho yao - TopicsExpress



          

Moja kati ya vyanzo vya mapato vya klabu ni makumbusho yao yanayoonesha kila kitu kuhusu klabu husika.Historia ya klabu,vikombe,wachezaji wa zamani,matukio muhimu nk.Sehemu za makumbusho za klabu zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza uchumi wa klabu mana watu toka sehemu mbalimbali huja kutembelea makumbusho hayo hasa kwa vilabu vyote vikubwa ,vya kati na hata vilabu vidogo kwa nchi za wenzetu.Mfano Real Madrid hutembelewa na watu c chini ya laki 4 na kuendelea kwa mwaka toka sehemu mbalimbali duniani kwenda kuangalia makumbusho ya klabu hiyo,vivyo hivyo kwa Man united,Arsenal,Barcelona,Juventus,Ac Milan nk Makumbusho kwa klabu pia ni hamasa kwa wachezaji wa vilabu husika kuwa wana jukumu kubwa la kuipigania timu wanayochezea.Leo hii mfano stempu za Mzee wng Jellah Mtagwa zilipaswa ziwe sehemu ya makumbusho ya ama TFF au ya Taifa kwa lengo ya kutuonesha sisi akina Edgar Kibwana ambao hatukubahatika kumuona wakati akicheza.Yanga na Simba sidhani km wana sehemu hz maalum za makumbusho ukizingatia kuwa vilabu hvy vilianzishwa miaka zaidi ya 70 iliyopita.Kuna namna nyingi za kuwa na vyanzo vya mapato wadau hasa kwa vilabu vyetu nchini.Nesema hvy kwa sababu wakati wa utambulisho wa mchezaji ISCO ktk klabu ya Real Madrid,Rais wa klabu hy Florentino Perez alionekana akimtembeza ISCO katika makumbusho ya klabu hy.
Posted on: Thu, 04 Jul 2013 10:10:05 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015