Mtu mwenye mali nyingi zaidi kuwahi kuishi katika historia ya - TopicsExpress



          

Mtu mwenye mali nyingi zaidi kuwahi kuishi katika historia ya binadamu alikuwa Mwafrika, Mansa Musa I. Wakati wa kifo chake mwaka 1331 alikuwa na mali zenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 400 za leo. Alikuwa mtawala wa dola ya Mali ambayo inajumuisha maeneo ya Ghana ya leo, Mali na Timbuktu. Mansa Musa I alifadhili miradi mingi katika eneo la Timbuktu zikiwemo maktaba na kabla ya uvamizi wa Ulaya barani Afrika himaya yake ilisimamia zaidi ya nusu ya biashara ya dhahabu na chumvi ya ulimwengu. Historia inaeleza kwamba Mansa Musa I alikwenda Mecca akiwa na msafara wa watu 70,000 na aligawa dhahabu nyingi kiasi kwamba bei ya dhahabu duniani ilishuka kwa miaka 10. Wakati Afrika ikitengeneza dola/himaya 8 zenye nguvu kabisa miaka hiyo, Ulaya ilikuwa katika zama za giza ikisumbuliwa na ukame, vita vya kikabila na vya kidini. Swali: Nini kimeikumbuka Afrika yetu kuwa kama ilivyo leo? Swali la msingi zaidi: Nini kifanyike kuirudisha Afrika kwenye zama za mafanikio kama enzi za Mansa Musa I na Timbuktu iliyostawi? Unaweza kusoma zaidi hapa kuhusu Mansa Musa na wengine: dailymail.co.uk/news/article-2218025/Meet-14th-Century-African-king-richest-man-world-time-adjusted-inflation.html
Posted on: Wed, 25 Sep 2013 15:29:33 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015